Sunday, November 18, 2012

MAJAMBAZI WALIOWAVAMIA MAPADRI WAMEKAMATWA.

WATU wanne akiwamo mwanamke mmoja wanaodaiwa kuwavamia na kuwajeruhi mapadri wawili kwa risasi na nondo mkoani Iringa, wamekamatwa.
Watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Ismani wanahusishwa na matukio mawili ya ujambazi uliofanyika katika Parokia za Kanisa Katoliki lililopo eneo la Kihesa Iringa Mjini na Parokia ya Isimani iliyoko Iringa Vijijini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda aliwaambia waandishi wa habari ofisni kwake jana kuwa watuhumiwa wote wamekamatwa kufuatia msako mkali uliofanywa na polisi baada ya tukio hilo lililsababisha watu watatu kujeruhiwa.
Alisema nyumbani kwa mwanamke ndiko walikuta bunduki iliyotengenezwa kienyeji inayodaiwa ilitumika katika ujambazi huo.
“Upekuzi uliofanyika nyumba kwa nyumba katika nyumba ya mwanamke ikipatikana gobore iliyotumika kutekeleza uhalifu huo. Nyumba ya mtuhumiwa mwingine motto wa mwanamke huyo zilipatikana gorori 37 na gramu 100 za baruti,” alisema.
Katika matukio hayo watuhumiwa wanadiwa kupora Sh4 milioni na Euro 100, huku wakiwashambulia kwa mapanga na risasi mapadri wawili, Padri Anjelo Burgio (66) wa Paroko wa Parukia ya Isamani na Msaidizi wake, Padri Herman Myala (36).
Mwingine aliyejeruhiwa kwenye matukio hayo ni Mlinzi wa Kanisa la Kiaskofu la Kihesa, Batholomeo Nzigiliwa.
Kamanda Kamuhanda alisema majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa  ya Mkoa wa Iringa na kwamba mlinzi wa Kanisa la Kihesa Nzigilwa hali yake ikielezewa kuwa ni mbaya.
Alisema mapadri  Burgio na Myala, wote wanaendelea vizuri.
Polisi wanaendelea kuwasaka watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo.

LOWASA AIHIMIZA SERIKARI KUTOA ELIMU BURE.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa, amesema wakati umefika kwa sasa hapa nchini elimu ya Sekondari iwe elimu bure na kumwondolea mwananchi wa kawaida mzigo wa kubeba gharama za elimu hiyo.
Lowassa akizungumza jana mjini Babati alisema, mjadala kuhusu elimu kutolewa bure hadi sekondari haukwepeki, hivyo kuwataka wadau wa elimu kuanza sasa kujadili suala hilo na kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapaswa kulifanya hilo kuwa moja ya ajenda zake katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Alisema elimu ya sekondari ikifanywa bure, itakuwa ni fursa kwa kila mtoto wa Kitanzania kuipata. Hatua ambayo itaongeza weledi na uelewa wa mambo mengi katika jamii.
“Ninasema sasa wakati umefika elimu ya sekondari kuwa kama elimu ya msingi kwa watoto kusoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne,” alisisitiza Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM).
Kwa kauli hiyo, Lowassa ni kama ameunga mkono Sera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao waliingia katika mgogoro na CCM kuhusu elimu kutolewa bure wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Chadema wamekuwa wakisisitiza kwamba elimu bure inawezekana hadi ngazi ya sekondari, lakini wakati wote CCM wamekuwa wakisema kuwa suala hilo haliwezekani na kwamba kauli za aina hiyo ni kuwahadaa wananchi.
Katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema, Dk Willibrod Slaa alitumia sera ya elimu bure kuanzia chekechea hadi sekondari kama kete ya kusaka ushindi, huku akisema chama chake kingetenga asilimia 35 ya bajeti kwa ajili ya kuboresha elimu na kutoa elimu bure.
Hata hivyo, aliyekuwa mgombea wa CCM na baadaye kupata ushindi, Rais Rais Jakaya Kikwete alikuwa akiwatahadharisha wapigakura kuwa kwamba ahadi ya Chadema ni hewa na kwamba hilo lisingewezekana.
Mvutano huo uliwaingiza makada wengine ambao ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye wakati huo alikuwa Meneja Kampeni wa CCM na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta na kwa upande wa Chadema, Dk Kitila Mkumbo naye alijitokeza kutetea sera ya chama chake.
Katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Novemba 10, 2010 katika Kata ya Mchangimbore katika Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, Rais Kikwete alisema “Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure” na kwamba lazima wananchi wachangie.
“Nimebahatika kukaa serikalini muda mrefu hiyo sera ya bure tulijaribu na ikatushinda na wakati huo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, tulikaa naye tukaona hilo haliwezekani tukaamua tubadilishe sasa nawashangaa wenzetu wanawadanganya eti watatoa bure.”
Kwa upande wake Dk Slaa akiwa mjini Arusha katika moja ya mikutano yake alisema kwamba CCM walikuwa wakipinga sera ya elimu bure hadi sekondari kutokana na kulea ubadhirifu na kuthamini anasa kuliko maendeleo kwa wananchi.
Jana akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Babati, Lowassa alisema wakati umefika kwa kila Mtanzania kuzungumzia suala hilo bila ya woga.

POLISI KENYA, WAENDELEA KUWASAKA WEZI WA MIFUGO.

Mifugo nchini KenyaBaada ya wizi wa mifugo uliotikea juzi nchini Kenya, Polisi wa nchi  bado wanaendelea na harakati za kuwasaka wezi wa mifugo waliosababisha mauaji ya takriban polisi 42 katika eneo la Baragoi kaskazini mwa nchi hiyo.
Polisi wengine zaidi ya 20 wanapokea matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta nchini humo. Maafisa hao wa polisi walikuwa katika harakati za kuwatafuta n'gombe walioibiwa wakati waliposhambuliwa na wezi wa mifugo.
Tayari polisi ya Kenya imetangaza vita dhidi ya wezi wa mifugo na maafisa kadhaa wa polisi wamepelekwa katika eneo hilo kuendeleza msako 

                                                                                       mkali wa majangili hao.

SAUT KUFANYA MAHAFARI JUMAMOSI HII

Jumamosi hii katika viwanja vya Raila Odinga katuka chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino, kutakuwa na shangwe nyingi kwa wahitimu wa chuo hicho kwa mwaka 2011/2012 kwani ndio watakapokuwa wanatunika vyeti vyao kwa ngazi ya Cheti na Shahada.

HALI BADO NI TETE HUKO GAZA

Al Jazeera's correspondent in Gaza will be on Reddit taking questions about the latest crisis to hit the Strip at 18:00 GMT

http://aje.me/U3r6SC

BASI LATEKETEA KWA MOTO NAIROBI

Ni baada ya kurushwa kwa guruneti hii leo jijini Nairobi,
 na watu watatu wamepoteza maisha

NAIROBI GURUNEDI  LILORUSHWA KWENYE BUS LAUA WANNE NA KUJERUHI WENGI. Serikali wanashuku kundi la Al-Shabaab.

The wreckage of a mini-bus ripped apart by an explosive in Nairobi's Eastleigh's estate on November 18, 2012. PHOTO / ZADOCK ANGIRA http://bit.ly/T9AGo0
PICTURE:Wreckage of Route 28 matatu after explosion

SERENGETI BOYS WAENDDELEA KUFANYA VIZURI.

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Congo Brazzaville katika mchezo uliochezwa leo uwanja wa Taifa. Bao pekee la Serengeti Boys limetiwa wavuni na beki Mudathir Yahya Abbas katika dakika ya 15 kwa mpira wa adhabu. Matokeo haya yanaifanya Serengeti Boys ihitaji ushindi au sare ya aina yoyote katika mchezo wa marudiano ili ifuzu kwenda Morocco katika michuano ya Afrika Mwakani.

Picha kwa hisani ya: http://bongostaz.blogspot.com/Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Congo Brazzaville katika mchezo uliochezwa leo uwanja wa Taifa.  
Bao pekee la Serengeti Boys limetiwa wavuni na beki Mudathir Yahya Abbas katika dakika ya 15 kwa mpira wa adhabu. Matokeo haya yanaifanya Serengeti Boys ihitaji ushindi au sare ya aina yoyote katika mchezo wa marudiano ili ifuzu kwenda Morocco katika michuano ya Afrika Mwakani.

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA IMETUA ARUSHA.

Jumapili Novemba 18, 2012: Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. John Nkolo (aliyesimama) akijitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Magesa Mulongo wakati Wajumbe wa Tume hiyo walipokwenda kujitambulisha kwake  kabla ya tayari ya kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya katika Mkoa huo. Wajumbe wengine ni Bw. Abubakari Ali, Bw. Ussi Ali na Bi. Mwantumu Malale. 
 Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. John Nkolo (aliyesimama) akijitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Magesa Mulongo wakati Wajumbe wa Tume hiyo walipokwenda kujitambulisha kwake kabla ya tayari ya kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya katika Mkoa huo. Wajumbe wengine ni Bw. Abubakari Ali, Bw. Ussi Ali na Bi. Mwantumu Malale.
Photo: Jumapili Novemba 18, 2012: Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mara baada ya wajumbe hao kujitambulisha kwake tayari kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya mkoani humo. Kutoka kushoto ni Bw. Abubakari Ali, Bw. Ussi Ali, Bi.  Mwantumu Malale (na wa kwanza kulia) Bw. John Nkolo. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mara baada ya wajumbe hao kujitambulisha kwake tayari kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya mkoani humo. Kutoka kushoto ni Bw. Abubakari Ali, Bw. Ussi Ali, Bi. Mwantumu Malale (na wa kwanza kulia) Bw. John Nkolo.
Photo: Jumapili Novemba 18, 2012: Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Mwantumu Malale akizungumza wakati wajumbe wa Tume hiyo walipokwenda kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha tayari kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Magesa Mulongo. Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Mwantumu Malale akizungumza wakati wajumbe wa Tume hiyo walipokwenda kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha tayari kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Magesa Mulongo.

KAMA ULIMISI, Haya ndio matokeo ya jana katika Barclays Premier League


Arsenal5 - 2Tottenham Hotspur

Liverpool3 - 0Wigan Athletic

Manchester City5 - 0Aston Villa

Newcastle United1 - 2Swansea City

Queens Park Rangers1 - 3Southampton

Reading2 - 1Everton

West Bromwich Albion2 - 1Chelsea

Norwich City1 - 0Manchester United

AY ASHIKILIA TUZO YA CHANEL O KWA AFRIKA MASHARIKI.


AY ndio msanii pekee kutoka TANZANIA (East Africa) aliyenyakuwa tuzo ya Channel O Music Video Award kwa mwaka huu 2012 katika kipengele cha MOST GIFTED AFRICAN EAST VIDEO OF THE YEAR. Video iliyochukuwa tuzo hiyo ni I DON'T WANT TO BE ALONE akiwa amewashirikisha wasanii kutoka Nairobi Kenya wanaokwenda kwa jina la Sauti Sol.

STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO TAR 18 NOVEMBER, ZIKO HAPA.

JESHI LA MONUSO LAINGIA GOMA

Mpiganaji wa M23 kaskazini ya GomaHelikopta zenye silaha za Umoja wa Mataifa zimeshambulia maeneo ya wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, huku mapambano yanaendelea baina ya jeshi la Congo na kundi la wapiganaji wa M23.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kuweka amani, Monusco, kimesema kuwa vikosi vya jeshi la serikali kaskazini ya mji wa Goma, vilishambuliwa Jumamosi asubuhi, na kufanya raia kulikimbia eneo hilo na helikopta za Umoja wa Mataifa kutumwa huko.
Monusco ina idhini ya kuwalinda raia na kuwasaidia wanajeshi wa serikali ikihitajika.
Hakuna idadi iliyotolewa ya maafa yaliyotokea.
Umoja wa Mataifa unazilaumu Rwanda na Uganda kwamba zinawaunga mkono wapiganaji - tuhuma ambazo nchi hizo inakanusha.

Zilizosomwa zaidi