Baada ya wizi wa mifugo uliotikea juzi nchini Kenya, Polisi wa nchi bado wanaendelea na harakati za kuwasaka wezi wa
mifugo waliosababisha mauaji ya takriban polisi 42 katika eneo la
Baragoi kaskazini mwa nchi hiyo.
Polisi wengine zaidi ya 20 wanapokea matibabu katika hospitali kuu ya
Kenyatta nchini humo. Maafisa hao wa polisi walikuwa katika harakati za
kuwatafuta n'gombe walioibiwa wakati waliposhambuliwa na wezi wa mifugo.
Tayari polisi ya Kenya imetangaza vita dhidi ya wezi wa mifugo na
maafisa kadhaa wa polisi wamepelekwa katika eneo hilo kuendeleza msako
mkali wa majangili hao.
mkali wa majangili hao.
No comments:
Post a Comment