Saturday, December 15, 2012

BAADHI YA MAENEO KUTOHAMIA DIGITAL

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewatoa
 hofu wananchi wote wanaoishi katika maeneo ambayo bado 
kufikiwa na mfumo mpya wa mawasiliano wa digitali, akisema
 wataendelea kupata mawasiliano kupitia mfumo wao wa zamani 
wa analojia.
 Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Meneja wa 
Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Innocent Mungi wakati akifafanua
 kuhusu wasiwasi uliojitokeza kwa wananchi hasa walioko mikoani.
Mungi alisema watazima mtambo wa zamani kule ambako huduma hiyo
 mpya ya digitali imefika, kwamba kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na
 mtambo huo, wataendelea kutumia televisheni zao kupitia mfumo wa zamani.
 Alibainisha kuwa, hadi sasa ni asilimia 24 sawa na mikoa 11 ya nchi ndiyo 
itafaidika na mawasiliano hayo ya digitali, ambapo kule kusikokuwa na mawasiliano hayo
 bado wataendelea kupata mawasiliano kwa kutumia satelaiti, madishi na usambazaji wa 
nyaya hadi hapo mfumo mpya utakapowafikia.

No comments: