1.AUSTIN
MORRIS A-40
AUSTIN
MORRIS A-40
|
Gari aina
ya Austin Morris A-40 lilitengenezwa
nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 – 1950. Ni gari la kwanza kutumiwa na Baba
wa Taifa na Rais wa kwanza Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwalimu
Nyerere alilitumia gari hilo toka mwaka 1955 – 1960 katika shughuli mbalimbali
za kuendeleza chama cha TANU likiendeshwa na dereva wake maarufu kwa jina la
SAID TANU. Baadaye Mwalimu Nyerere alilikabidhi gari hilo kwa vijana wa TANU kwa
kazi za chama kabla ya kupelekwa Makumbusho ya taifa na kuwa sehemu ya Historia
ya Tanzania.
2. AUSTIN
MORRIS (A-40 VAN GUARDS)
AUSTIN MORRIS (A-40 VAN GUARDS) |
Gari aina ya
Austin Morris A-40 maarufu kama Van Guards lilitengenezwa kati ya miaka ya 1945
– 1950. Gari hili lilitumiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa
shughuli za TANU akiwa Dar es Salaam na ziara za mikoani kuhamasisha shughuli
za chama. Dereva wake alikuwa ni SAID TANU.
3.ROLLS
ROYCE
ROLLS ROYCE |
Gari aina ya
ROLLS ROYCE lilitengenezwa 1938 na
kuletwa na Gavana wa wakati huo Harold Mac Michael katika utawala wa wakoloni
waingereza na lilitumiwa na Gavana wa mwisho kuitawala Tanganyika Sir Richard
Turnbull.
Rolls Royce lilitumika
kupokea wageni mbalimbali waliotembelea Tanganyika wakati huo wakimwemo Rais wa
zamani wa Liberia Hayati William Tubmann na Mfalme wa zamani wa Ethiopia Hayati
Haille Sellasie.
Gari hilo
lilitumika hadi mwaka 1962 baadaye mwaka
1978 Rais wa kwanza Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere aliagiza Rolls
Royce kuhamishwa toka Ikulu hadi Makumbusho ya Taifa. Kwa sasa ni sehemu ya Historia ya Taifa la Tanzania.
4. ROLLS
ROYCE (PHANTOM V)
ROLLS ROYCE (PHANTOM V) |
Gari aina ya
Rolls Royce Phantom V lilitengenezwa nchini Uingereza na kutolewa na nchi hiyo
kwa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Novemba
05,1965.
Rolls Royce Phantom V lilianza kutumika mwaka 1970 kwa
kupokea viongozi wa nchi mbalimbali wakiwemo Marais na mabalozi wa nchi
mbalimbali waliotembelea Tanzania.
Gari hilo
lina sifa za kipekee kwa wakati huo likionekana la kisasa zaidi kwani lina sehemu ya mbili za
kuweka bendera, moja upande wa kulia ambako aliketi mgeni na upande wa kushoto
bendera ya Tanzania alikoketi mwenyeji wake (Mtanzania).
Sehemu ya
juu ya Rolls Royce Phantom V yaweza
kufunguliwa kwa minajili ya kuwaruhusu viongozi kusimama na kuwapungia
mikono
wananchi au kuruhusu hewa kuingia hasa wakati wa joto (hapa ni kama
AC/kiyoyozi kwa magari ya sasa). Kwa kweli tumetoka mbali na huu ndio
uhondo wa historia.
Rais wa
awamu ya pili wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi alilitumia gari hilo na Rais
wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa akalitumia pia kabla ya
kuamua kulipeleka Makumbusho ya Taifa Machi 08,2006 na kuwa sehemu ya Historia ya
Tanzania.
5.MERCEDEZ
BENZ 230.6
Mercedez
Benz 230.6 lilijulikana kama gari la jumuiya kwani lilitumiwa na Rais wa
Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere kwa shughuli za jumuiya Afrika Mashariki iliyoundwa mwaka 1967 na nchi
za Tanzania, Kenya na Uganda ambapo kila nchi ilikuwa na gari kama hilo.
Moja ya sifa
ya gari hilo kwa wakati huo ni kuwa na uwezo wa kubeba watu wengi zaidi.Uwezo
wake ni kubeba marais wageni wawili, mpambe wa Rais, mwandishi habari wa Rais na
Rais mwenyeji kwa mara moja.
Mercedez
Benz 230.6 lilikuwa na namba za kipekee ambazo ni RE-1 (yaani Royal Excellecy 1).Hata
hivyo Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki ilidumu kwa miaka 10 tu (1967 –
1977) ambapo ilivunjika kwa sababu mbalimbali. Gari hilo likapelekwa Makumbusho ya Taifa Oktoba
mwaka 2002 na kuwa sehemu ya Historia ya Tanzania.
MERCEDEZ
BENZ E 300
Mercedez
Benz
E 300 lilitengenezwa nchini Ujerumani na kununuliwa na serikali ya Tanzania
Desemba 17, 1996 ambapo Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alilitumia kwa shughuli za kitaifa na binafsi
katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani baada ya kustaafu Urais.
MERCEDEZ
BENZ E 300
|
Mercedez
Benz E-300 litaendelea kukumbukwa zaidi kwani ndilo gari la mwisho kwa Hayati
Mwalimu Nyerere kulitumia enzi za uhai wake hapa nchini kwani alilitumia kwa
mara ya mwisho kabisa Agosti 31,1999 akienda kupata matibabu huko nchini
Uingereza.
Alisafiria
gari hilo kutoka nyumbani kwake Msasani hadi uwanja wa kimataifa wa Dar es
Salaam (kwa sasa Mwalimu Julius Nyerere).
Hata hivyo
kwa MASIKITIKO MAKUBWA Baba wa Taifa hakurudi tena kulitumia tena gari hilo
kwani alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999 katika hospitali ya Mtakatifu Thomas
huko nchini Uingereza. MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI,AMEN.
Gari lake
alilotumia kwa mara ya mwisho (Mercedez
Benz E 300) likatolewa na mkewe Mama Maria Nyerere kwa ajili
ya kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa Septemba 24, 2004.
Katika
utalii wa ndani tumeangazia kipengele kidogo tu cha usafiri kwa kuangalia
magari aliyotumia Rais wa kwanza Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wenzake hivyo kama Watanzania
nadhani kuna mambo mengi ya kujifunza kupitia utalii wa ndani hasa wa
Kiutamaduni na kuangalia historia mila na desturi za Watanzania kabla na wakati wa ukoloni hatimaye baada ya Uhuru.
Kuna mambo mengi ambayo
Watalii kutoka nchi za nje wanayafahamu kuliko Watanzania wenyewe. Mathalani,
mtu wa Bagamoyo hajui historia ya mji wa kale ya Kaole, Caravan Serai na
mengineyo huku mtu wa Dar es Salaam akishindwa kufika Makumbusho ya Taifa
jijini humo au kijiji cha Makumbusho Kijitonyama kujua Historia
mbalimbali. Vivyo hivyo, Mtanzania anayeishi Mikumi, Kilimanjaro au Serengeti
anashindwa kujua mambo yanayomzunguka huku mtu kutoka Ujerumani au Marekani
anafahamu mengi kuhusu maeneo. Hii ni changamoto kubwa kwa Watanzania.
Kuna watu
wanasema umasikini wa kipato lakini wale wanaozunguka maeneo hayo mara nyingi
viingilio ni bei ambayo Mtanzania anaweza kumudu mathalani shilingi elfu miatano (1500)
kuingia katika Makumbusho ya Taifa, ukitoka Magomeni jijini utatumia nauli
shilingi 600 kwenda na kurudi maeneo ya Posta. Ni ukweli usiopingika kuwa uchumi umeyumba kwa wananchi lakini mwananchi
huyo huyo ana uwezo wa kununua bia 3 – 5 kila siku lakini hana uwezo wa
kugharamia shilingi elfu 1500 au 5000 kwa kutembelea kivutio kimojawapo karibu
na anapoishi angalau mara moja kwa mwaka. ….huenda kuna lingine zaidi ya kipato.
Afisa Elimu
wa Makumbusho ya Taifa Mawazo Ramadhani anasema mwamko wa watanzania ni mdogo
hasa utalii wa kiutamaduni huku akikiri kupokea makundi makubwa ya wanafunzi wa
shule za msingi, sekondari na vyuo na wageni kutoka nje.
Utalii wa
kiutamaduni unahusisha vitu ambavyo mwanadamu anavizalisha kila siku mavazi,mila
na desturi za jamii ya watanzania.
Hata hivyo
Afisa elimu huyo amesema katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakipokea
watalii wa ndani hasa familia katika siku za wikiendi na sikukuu jambo
linalotia faraja kwa kiasi kikubwa katika sekta hiyo.
Kila la heri kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kila la heri kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Naomba
kuwasilisha.
No comments:
Post a Comment