Kocha
mkuu wa timu ya Young Africans Sports Club, Mholanzi Ernie Brandts
amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili timu ya Polisi Morogoro
katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom utakaofanyika kesho uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Akiongea katika mtandao wa klabuhiyo leo
asubuhi katika mazoezi yaliyofanyika shule ya sekondari Loyola, amesema
wachezaji wake wote wapo safi, wana ari ya mchezo na ushindi, hivyo
anaamini mchezaji yoyote atakayempanga atafanya vizuri.
Polisi
Morogoro timu iliyoipanda ligi msimu huu 2012/2013 inakamata mkia
katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom ikiwa na pointi 2 ilizozipata kwa
kutoka sare michezo miwili kati ya michezo saba iliyokwishacheza.
Yanga
ambayo mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya
timu ya Ruvu Shooting katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki,
itaingia uwanjani kusaka pointi 3 muhimu zitakazo isogeza mpaka nafasi
tatu za juu na kupunguza tofauti ya point na mtani wake wa jadi Simba
anayeongoza ligi kwa pointi 19.
Katika mazoezi
yaliyofanyika leo asubuhi, kocha Brandts ameendelea kufurahia kuwepo kwa
wachezaji wake wote, kitu kitakachopelea kumtumia mchezaji yoyote
atakayetaka kumtumia kwa mchezo huo wa kesho, kwani hakuna mchezaji
aliye majeruhi .
Vijana wa jangwani kwa sasa
wanakamata nafasi ya tatu katika msimao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara kwa kufikisha point 14 nyuma ya Azam yenye pointi 17 na Simba yenye
pointi 19 ikiwa mbele kwa mchezo mmoja.
Mchezo utaanza majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na viingilio vya mchezo huo ni:
VIP A 20,000/=
VIP B &C 15,000/=
Orange 8,000/=
Blue & Green 5,000/=
No comments:
Post a Comment