Saturday, December 15, 2012

KITUO CHA POLISI CHACHOMWA MOTO, POLISI WAWILI WAFARIKI HUKO NGARA

VITENDO vya wananchi kujichukulia sheria mikononi vinaendelea kushika kasi ambapo askari wawili wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, wanadaiwa kuuwa na wananchi wenye hasira kali jana.
Mauaji hayo yalifanyika baada ya wananchi hao kuvamia na kukichoma moto kituo cha polisi cha Mugoma wilayani humo baada ya askari hao kudaiwa kumpiga risasi fundi wa pikipiki.

Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilitokea mchana wakati askari kadhaa wa kitengo cha usalama barabarani walipofika kwa fundi pikipiki huyo na kutaka kuichukua pikipiki aliyokuwa akiitengeneza kwa madai kuwa ilikuwa na makosa.Kwamba fundi huyo aligoma na kueleza kuwa asubiriwe mwenye pikipiki ili kuepuka kudaiwa chombo hicho cha usafiri.

Mmoja wa mashuhuda hao, aliyatambulika kwa jina moja la Libela, alidai kuwa baada ya mvutano wa muda mfupi, askari hao walifyatua risasi na kumpiga fundi huyo mguuni na kifuani, hivyo kusababisha kifo chake.
Aliongeza kuwa, tukio hilo liliwapandisha hasira wananchi na kuwafukuza askari hao waliokimbilia katika kituo hicho cha polisi.

Lebela alifafanua kuwa, wananchi hao waliamua kukichoma moto kituo hicho hatua iliyosababisha askari waliokuwemo kutoka na kukimbia kila mmoja na muelekeo wake.

Alisema kuwa askari aliyetajwa kwa jina la Koplo Paschal alianguka wakati akijinusuru, hivyo kuvamiwa na wananchi waliokuwa na zana mbalimbali za jadi ambazo walitumia kumshambulia na kumuua papo hapo.
Wananchi hao pia wanadaiwa kumfuata askari mwingine anayetajwa kwa jina la Pc Alex aliyekuwa amekimbilia kwenye nyumba ya mwananchi mmoja na kumtoa kwa nguvu na kisha kuanza kumshambulia hadi kumuua.
STORY na Mbeki Mbeki,

No comments:

Zilizosomwa zaidi