Thursday, April 18, 2013

HAPA NI BAADA YA LISU KUTIMULIWA KATIKA UKUMBI WA BUNGE HAPO JANA.

 
Tundu Lissu
Naibu Spika Ndugai jana  aliamuru Mbunge wa Jimbo la Singida Vijijini na Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,Tundu Lissu atolewe nje ya Bunge huku wabunge wa upinzani wakizomea na kusema hatoki mtu. 

Amri hiyo ilitokaea baada ya Lisu  kuingilia kati mchango wa Mwigulu Nchemba aliyesema kwamba udini ni jambo geni hapa nchini....
 Tanzania imeongozwa na CCM tangu uhuru, na marais wote wamekuwa wakitoka CCM, rais wa kwanza alikuwa mkristo, wa pili muislam, wa tatu mkristo na wa nne ni muislam..akasema kama udini ni jambo geni watanzania tujiulize limekujaje? Kwanini sasa na sio wakati huo?

Akasema katika kampeni za urais 2010 Dr Slaa akiwa katika kampeni mkoani singida alitumia viongozi wa dini kufanya vikao vya kampeni badala ya kutumia wanachama wa chama chake...na viongozi hao wapo tayari kutoa ushahidi...
Ndipo Tundu Lissu aliposimama na kuomba mwongozo, spika akamwambia atulie kwa sababu Susan Kiwanga tayari amepewa nafasi akalisemea hilo na muda ni mdogo Lissu akang'ang'ania ndipo Naibu Spika akaamuru askari amtoe nje Lissu.

Pamoja na hayo Naibu spika amewafungia vikao vitano kinyume na kanuni za Bunge Mh. Lema, Mh. Mbilinyi. Mh. Kiwia, Mh. Msigwa, Mh. Wenje

No comments:

Zilizosomwa zaidi