HUKUMU ya Kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya
maandamano haramu bado iko njia panda baada ya kuaahirishwa mpaka tarehe 9 mei mwaka huu.
Kesi hiyo imeharishwa baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa ,kutokuwepo Mahakamani hapo.
Awali hakimu huyo alitarajiwa
kuketi katika kiti cha enzi na kutoa hukumu ya kesi hiyo Na.245/2012
inayomkabili Ponda na wenzake.
Aprili 3 mwaka huu, Mawakili wa
upande wa Jamhuri ,Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi
Juma Nassor na Njama waliwasilisha majumuisho yao mahakamani hapo kwa
njia ya maandishi ambapo mawakili wa upande wa jamhuri waliiomba
mahakama iwaone washitakiwa wote wana hatia na wapewe adhabu kwa mujibu
wa sheria.
Wakati mawakili wa utetezi waliiomba mahakama iwaone washitakiwa
hawana hatia na iwaachilie huru kwa sababu hawakutenda makosa
yanayowakabili na kwamba upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi
yao.
No comments:
Post a Comment