Saed Kubenea (Kushoto) |
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam hapo jana imetoa hukumu ya kesi namba 28 ya
mwaka 2014 ambayo iliitaka mahakama hiyo kutoa tafsri sahihi ya mamlaka
na mipaka ya Bunge maalum ya katiba iliyofunguliwa na mwandishi wa
Habari Saed Kubenea.
Akisoma
hati ya amri ya mahakama Jaji Augustino Mwarija kwa niaba ya majaji
watatu waliosikiliza shauri hilo,amesema kumekuwepo na Utata katika
kifungu cha 25(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011
katika lugha mbili zilizotumika kuandika sheria hiyo. Na kusema kuwa
kutokana na kifungu hicho kinaipa mamlaka bunge maalumu la Katiba
kuijadili rasimu ya katiba,kubadili au kuboresha na kuwa Bunge hilo
lina mipaka kwa kuzingatia kifungu cha 9(2) cha sheria ya mabadiliko ya
katiba.
Akizungumza baada ya amri hiyo nje ya mahakama kuu Wakili wa Saed
Kubenea, Peter Kibatala amesema wanafurahi kuona mahakama imetoa
maamuzi kwa wakati na kueleza kuwa tasfiri iliyotolewa ni katika
kusaidia wananchi kupata katiba iliyotokana na maoni yao.
Katika kesi hiyo, Kubenea aliiiomba mahakama itoe tafsiri sahihi ya
Mamlaka ya Bunge la Katiba kwa kuzingatia kifungu cha 25 (1) na (2) cha
Sheria ya Marekebisho ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011. na kuiomba
Mahakama itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya
Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
No comments:
Post a Comment