Naibu katibu
mkuu wa Taifa wa CHADEMA
Zito Kabwe amekanusha
uvumi ulioenea wa kuwa amemuowa mtoto wa Rais Kikwete na ndio maana amepunguza makali yake
Bungeni ya kuuliza maswali na kuchangia hoja
Zito alitowa kauli hiyo ya kukanusha uvumi wa kumuowa mtoto wa Rais Kikwete hapo jana
juzi wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mpanda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
viwanja vya Maridadi mjini hapa
Alisema uko uvumi ambao umeenea hapa
nchini kuwa makali yake yamekupungua bungeni kutokana na yeye kumuowa
mtoto wa Rais Kikwete wakati
sio kweli yeye hajamuowa mtoto wa
Kikwete
Alifafanua
kuwa yeye Bungeni hayuko kwa ajiri ya
kupigana ngumi bali yeye siku zote toka amekuwa mbunge amekuwa
akipigania kutoa hoja zenye nguvu
ndani ya Bunge kama hana hoja za
msingi huwa hakulupuki ovyoovyo
Alieleza ndio
maana katika kikao kijacho cha
Bunge ameisha wasilisha
maombi ya mswada binafsi wa kupendekeza kufutwa
kwa sheria ya mwaka 1976 sheria
namba 3 ambayo amedai inavinyima haki na uhuru vyombo vya habari
Wako
viongozi wamekuwa wakiitumia vibaya
sheria hiyo na hasa pale wanapo kuwa
wamekosolewa au kuandikwa vibaya na
magazeti mbona mie Zito nilikuwa naandikwa
vibaya na kusingiziwa kuwa
nimejenga nyumba ya gorofa Dodoma wakati hata kiwanja sina Dodoma lakina
hata siku moja sija vichukia vyombo vya habari
alisema Zito
Alisema kitendo
cha kuyafungia magazeti ya Mtanzania na Mwananchi ni ukiukwaji wa
katiba kwani kila mwananchi ana haki ya kupata habari na kitendo
hicho kinapunguza ajira kwa vijana
Alisema leo hii
Serikali inapenda kufanya mambo yake
kisiri na ndio maana hata mishahara yetu
sisi wabunge ambao mmetuchagua nyinyi wananchi hamjuwi wakati ni haki
yenu ngoja niwatajie mshara anao pata waziri na Wabunge
Mshahara wa Mbunge kwa mwezi anapa kwa mwezi shilingi
Tsh 11,200,000 wakati waziri mkuu
anapata mshara wa shilingi milioni 26 kwa mwezi na kila kitu anapata bure kama ni kosa
kutamka mshahara wa ni kosa basi
namie nichukuliwe hatua kama
magazeti yalivyo fungiwa na kesho nikiwa Wilayani Sikonge ntataja na Rais anapata mshahara kiasi
gani kwa mwezi
Kuhusu katiba
aliomba marekebisho ya katiba yazingatie
zaidi kuwapa mamlaka ya maamuzi wananchi
kuliko viongozi kama ilivyo sasa na alishauri mbunge awe mbunge tuu na asiwe
waziri kwani mbunge anapo kuwa waziri matokeo yake ni wananchi waliomchagua wanakosa
uwakilishi bungeni
Alisema anao mfano hai kwa
Waziri Mkuu Mizengo Pinda toka
amechaguliwa kuingia Bungeni mwaka 2000 hajawahi kuuliza swali hata moja bungeni kama
kuna mtu anaushahidi wa swali lolote ambalo Pinda aliwahi
kuuliza yeye Zito yuko tayari kumpa shilingi laki mbili
mwananchi huyo
Alifafanua kuwa
Pinda alichaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza na aliteuliwa kuwa
naibu wa Tamisemi hivyo nafasi hiyo ya uwaziri imembana muda
wote kuuliza maswali.
No comments:
Post a Comment