Tuesday, September 24, 2013

UHURU KENYATTA ATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO NCHINI KENYA..

Baada ya vyombo vya usalama nchini Kenya kufanikiwa kuwaondoa wanamgambo wa Al shabaab  ambao walivamia na kuliteka eneo la West Gate na kusababisha vifo vya takribani watu 72, sasa Rais wa Nchi hiyo Bw.Uhuru Kenyatta ametangaza siku tatu za maombolezo kwa kuwa nchi imekuwa katika wakati mgumu tangu siku ya jumamosi ambapo shambulio hilo la kugaidi lilichukua nafasi.

Katika kulikomboa eneo hilo la West Gate, vyombo vya usalama vimefanikiwa kuwaondoa wanamgambo wote waliokuwa wamesalia ndani ya jengo hilo na kufanikiwa kuwaua wanamgabo watano wa kikundi hicho cha kigaidi cha Al shabaab.

No comments: