Msanii mkongwe katika
anga ya muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes akiwaimbisha mashabiki wake
kibao waliofurika vilivyo ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi ambapo tamasha la Serengeti fiesta linafanyika.
Kundi
la Weusi likiongozwa na Joe Makini wakilishambulia jukwaa usiku huu
kwenye tamasha la serengeti fiesta uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Mwanadada aliyewahi kufanya vyema kwenye shindano la BSS,Menina akiimba kwa hisia jukwaani
Mkali
mwingine wa bongofleva anaefanya vyema kwenye muziki huo,akitambulika
kwa jina la kisanii Ney wa Mitego akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu
kwenye wakati wa tamasha la serengeti fiesta likiendelea kwenye uwanja
wa Majengo,mjini Moshi.
Mwanadada
Linah akimpagawisha shabiki wake vilivyo jukwaani usiku huu ndani ya
tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Mkali
wa shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu
kwenye tamasha la serengeti fiesta ndani ya uwanja wa Majengo mjini
Moshi.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya ambaye amekuwa akifanya vyema tangu aibuliwe
na Serengeti supa Nyoya kutoka jijini Mbeya,Neylee kwa sasa anakula
matunda ya ufanisi wake wa kisanii katika anga ya muziki huo,pichani
akiwa kwenye jukwaa la serengeti fiesta usiku huu mjini Moshi kwenye
uwanja wa Majengo ambapo tamasha hilo likiendelea.
Pichani
kati ni msanii wa bongofleva kutoka nyumba ya vipaji THT,Ally Nipishe
akiwa na madansa wake wakilishambulia jukwaa la fiesta usiku huu.
Mzee wa masauti kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Acudo,Christian Bella akiimba jukwaani.
Sehemu ya umati wa watu kutoka mjini Moshi wakiwa kwenye tamasha la fiesta usiku ndani ya uwnaja wa Majnego.
Mwanamuziki wa bongofleva kutoka THT,pichani kati Linah akicheza kwa madaha kabisa na madansa wake jukwaani usiku huu.
Mwanadada aliyewahi kufanya vyema kwenye shindano la BSS,aitwaye Menina akiimba jukwaani na madansa wake.
Wasanii
wanaounda kundi la Jambo Skwadi wakilishambulia jukwaa kwa namna ya
kipekee kabisa usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta
linalofanyika kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.
No comments:
Post a Comment