Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa
Penina Mlama kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa
kipindi cha miaka mitatu ijayo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Idara ya Habari – MAELEZO leo, Uteuzi huo wa Profesa Mlama unanzia mwaka
2013 na unatarajia kumalizika mwaka 2016.
Prof. Mlama ni Profesa wa Sanaa na Sanaa za Maonyesho Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara ameteua jumla watu 12 kuwa wajumbe wa BASATA kwa
kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka huu.Walioteuliwa ni pamoja
na wawakilishi wa Vyama na Asasi mbalimbali wa Baraza hilo ambao ni Dkt.
Vincensia Shule, John Kitime , Angela Ngowi, Dkt. Herbert Makoye, Erick
Shigongo na Alex Msama.
Wawakilishi wengine ni pamoja na Juma Adam Bakari, Daniel Ndagala,
Michael Kadinde na Joyce Fisoo. Wanaoingia kwa mujibu wa nyadhifa zao ni
Prof. Hermas Mwansoko na Katibu Mtendaji wa BASATA.Katika hatua
nyingine Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara amemteua Bwana Ghonche Materego kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Kabla ya uteuzi huo Materego alikuwa amemaliza muda wake kama Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa.Wajumbe wa Bodi hiyo walioteuliwa
na Waziri Mukangara ni Dkt. Herbert Makoye, Prof. Emanuel Mbogo, Dkt.
Lucy Mboma, Prof. Hermas Mwansoko pamoja na Katibu Mtendaji wa
BASATA.Wakati huo huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dkt. Fenella Mukangara ameteua jumla ya watu 21 kuwa wajumbe wa Baraza
la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia
mwaka 2013 hadi 2015.
Wajumbe hao ni Dkt. Shani Omari, Prof. Yohana Msangila, Ester Riwa,
Dkt. Issa Zidi, Khadija Juma na Dkt. Martha Qorro.Wengine ni Mmanga
Mjawiri, Razia Yahaya, Richard Mbaruku, Selina Lyimo, Keneth Konga,
Amour Khamis, John Kiango, na Shani Kitogo.Wajumbe wengine ni Ally
Kasinge, Ahmed Mzee, Rose Lukindo, Shabani Kisu pamoja na Edwin
Mgendera.Taarifa hiyo imefafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo la
BAKITA atachaguliwa na wajumbe watakapokutana kwenye kikao chao cha
kwanza.
No comments:
Post a Comment