Rais Dkt Jakaya
Kikwete, anatarajiwa kuanaanza ziara ya kiserikali ya siku nane Mkoani Mwanza,
ambapo atakagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, iliyotekelezwa na
serikali ikiwa ni utekelezwaji Ilani ya Uchaguzi ya CCM .
Rais ambaye atawasili
jijini hapa leo asubuhi,
baadaye ataelekea nchini Uganda kukutana na Rais wa nchi hiyo, Yoweri
Mseven, kabla ya kurejea jijini Mwanza Alhamisi kwa ajili ya kuanza ziara
ya siku saba
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, Rais Dkt
Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa wa Mwanza kujionea shughuli za
maendeleo, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kufungua miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Injinia Ndikilo
alizitaja shughuli hizo kuwa ni miradi ya Nishati ya Umeme wa Millennium
Challenge Cooperation (MCC) unaofadhiliw na serikali ya Marekani uliotekelezwa
katika wilaya za Misungwi, Magu, Nyamagana, Ilemela na Sengerema ambapo
utazinduliwa katika Kijiji cha Bukokwa.
Mkuu wa Mkoa alifafanua
kuwa, katika sekta ya afya, Dk Kikwete atafungua jengo la Zahanati ya Lugeye
wilayani Magu, Maabara ya Hospitali ya wilaya ya Ukerewe na kuzindua X-ray
mbili ikiwemo kubwa ya kisasa iliyotolewa na Denmark kwa ufadhili wa
Mbunge wa jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga.
Akiwa Misungwi katika
sekta ya Afya atazindua pia E-xray ndogo iliyonunuliwa na Halmashauri ya
wilaya ya Misungwi kwa ajili ya Hospitali ya Mitindo ya wilaya hiyo na kufungua
Shule ya Msingi ya Kisasa, Ntulya iliyojengwa na NGO ya Afrian School House ya
Marekani kupitia Mbunge huyo.
Miradi mingine ni ya
Ulinzi na Usalama ambapo atafungua Kituo kipya cha Polisi Nyakato Jijini hapa,
mradi wa maji wa Katunguru Wilayani Sengerema, uwanja wa ndani wa michezo Malya
Wilayani Kwimba na kuweka jiwe la Msingi katika Kanisa la Kisabato Pasiansi
Wilayani Ilemela.
Wakati wa ziara hiyo
katika maeneo atakayotembelea Rais, atazungumza na wananchi hivyo injinia
Ndikilo ametoa natoa wito kwao kujitokeza
kwa wingi kumpokea na kumsikiliza, hii ni fursa ya pekee kwa wananchi wa Mkoa
wa Mwanza kujionea shughuli za maendeleo yao zilizvyotekelezwa na serikali yetu
kama utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha kuanzia 2010 hadi
2015 nchini kote.
No comments:
Post a Comment