Ulinzi mkali katika mpaka wa Sinai |
Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari limelipuka nje ya makao makuu ya ujasusi na kuwaua watu wanne.
Duru zinasema kuwa watu wanne wamejeruhiwa
kwenye shambulizi hilo karibu na eneo la Rafah, kwenye mpaka wa Misri na
ukanda wa Gaza.
Mlipuko wa pili ulilenga kuzuizi cha jeshi. Haijulikani ikiwa mtu yeyote alijeruhiwa.
Eneo la Sinai limekumbwa na mashambulizi mengi
yanayofanywa na wapiganaji wa kiisilamu tangu jeshi kumwondoa mamlakani
rais Mohammed Morsi mapema mwezi Julai.
Mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliendesha gari
kwa kasi sana na kugonga jengo hilo. Liliporomoka huku baadhi ya
wanajeshi wakikwama chini ya vifusi, kwa mujibu wa shirika la habari la
AP.
Walioshuhudia shambulio hilo wanasema kuwa mlipuko mkubwa uliharibu madirisha ya jengo hilo katika eneo la Imam Ali mjini Rafah.
Punde baadaye, wanamgambo walilenga kizuizi cha jeshi barabarani kwa kuwafyatulia maguruneti.
Msako wa jeshi
Mashambulizi hayo yametokea siku chache baada ya
angalau wapiganaji tisa kuuawa katika operesheni kubwa ya kijeshi,
karibu na miji ya Rafah na Sheikh Zuweyid.
Mnamo tarehe 7 Septemba, helikopta za jeshi
zilifanya mashambulizi ya angani, yaliyonuia kuharibu silaha , magari na
maficho ya wapiganaji, katika kile kilichosemekana kuwa operesheni
kubwa zaidi ya kijeshi kuwahi kushuhudiwa katika eneo hilo.
Jeshi limetuhumu bwana Morsi kwa kuwa mpole sana
kwa harakati za wapiganaji, baada ya kuwaachilia wafungwa waliohusika
katika harakati za makundi ya wapiganaji wa kiisilamu.
No comments:
Post a Comment