KAMATI ya Taifa inayohusika na mazishi
ya aliyekuwa waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa imetoa ratiba ya
mazishi ambapo mwili wa marehemu utawasili siku ya jumamosi tarehe nne
saa saba mchana katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Terminal II na
kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni B jijini Dar es salaam. (HM)
Akizungumza na waandishi wa habari
jana Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) Dk.
William Lukuvi alisema kamati itakayohusika na mapokezi ya mwili wa
marehemu ni ofisi ya Waziri Mkuu itakayohusika na ndugu, viongozi na
wananchi na Kamati ndogo ya mkoa wa Iringa inayoongozwa na mkuu wa mkoa
huyo Dk. Christine Ishengoma.
Dk. Lukuvi alisema siku hiyo ya
jumamosi saa kumi na moja jioni mwili marehemu utapelekwa katika
hospitali ya Lugalo na tarehe tano siku ya jumapili saa tano na nusu
asubuhi mwili wa marehemu utapelekwa katika ukumbi wa Karimjee kwa ajili
ya ibada na kutoa heshima za mwisho.
Alisema ifikapo saa nane mchana mwili
wa marehemu Dk. Mgimwa utapelekwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere
Terminal I kwa ajili ya kuelekea Mkoa wa Iringa.
Ifikapo saa kumi kamili alasiri mwili
wa marehemu utakuwa umewasili Mkoa wa Iringa katika uwanja wa ndege
Nduli na kuagwa na viongozi na wananchi wa mkoa huo katika ukumbi wa
Siasa kilimo na baada ya hapo utapelekwa kijijini kwake Magunga.
Waziri Lukkuvi alimalizia kwa kusema
kuwa shughuli za mazishi ya Marehemu Dk. Mgimwa zitafanyika 6.1.2014
kuanzia majira ya saa sita mchana katika kijiji cha Magunga mkoani
Iringa na atazikwa kwa heshima zote za Kiserikali. Chanzo: Kiza Sungura-
MAELEZO Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment