TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII
Baada ya kufika Kisesa jana mara baada ya
kusikia mauaji ya kutisha ya Diwani wa kata ya Kisesa na aliyepata kuwa
mwenyekiti wa CCM MKOA WA MWANZA MH CLEMENCE MABINA,ili kushuhudia tukio
hilo la kusikitisha,nilipata shida kufika eneo ambalo tukio la mauaji
lilotokea kijiji cha Kanyama, kila aliyeulizwa alichukia kuhusu kifo
hiki, hakuwa tayari kusema neno, hapa ndipo umauti ulipomfika Mzee
Mabina, mashuhuda walisema kuwa kifo hiki kilitokana na
mgogoro wa umiliki wa mlima kanyama ambako kuna vijana hujihusisha na
uvunjaji wa mawe,mara baada ya Mh Mabina kununua eneo hilo ndipo mgogoro
kati ya wananchi na MZEE MABINA ULIPOANZA,Taarifa nilizozipata,zinasema
Mzee Mabina alikuwa amewatuma vijana wake kwenda kuweka alama za mipaka
kwenye huo mlima wa Kanyama, vijana wake walikuta wanakijiji wakiendelea
na kazi kwenye Mlima Kanyama,wanakijiji wakawazuia vijana wa Mabina
kuweka alama kwa madai kuwa huo mlima ni mali ya kijiji,Marehemu Mabina
alilazimika kwenda huko akiwa na silaha ya moto,alipofika wanakijiji
walianza kumshambulia kwa mawe huku nae akiwakabili kwa silaha ya moto
aliyokuwa nayo,katika mapambano hayo silaha ya moto ya Mzee Mabina
ilisababisha umauti wa kujana mmoja!Mzee Mabina wakati anawakimbia
wanakijiji hao,alidondoka na wanakijiji kumfikia na kumpiga kwa mawe na
kusababisha umauiti!..MGOGORO WA ARDHI NA MOB JUSTICE UMESABABISHA KIFO
CHA MZEE MABINA!Nimedokezwa kuwa mgogoro huu ni wa muda mrefu,kwa nini
haukutatuliwa mpaka unafikia kiwango cha watu kupoteza maisha?kwa nini
tunafumbia macho migogoro ya ardhi mpaka inasababisha mapigano?
Na Emmanuel Dotto
No comments:
Post a Comment