Unyama zaidi umebainika katika taarifa
ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu
Operesheni Tokomeza Ujangili baada ya kubainika kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Ulanga mkoani Morogoro, Francis Miti, kukiri kujihifadhi kwenye hoteli
moja nje ya wilaya yake.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, James
Lembeli akisoma ripoti hiyo bungeni juzi alisema Operesheni Tokomeza
Ujangili, ilisababisha hofu miongoni mwa wananchi na viongozi na baadhi
yao kuyakimbia makazi. Lembeli alisema watuhumiwa, walikamatwa,
walipekuliwa na kudhalilishwa na baadhi kutojulikana walipo.
"Baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi,
madiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji na watumishi wa Serikali,
walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza,"
"Watuhumiwa waliokamatwa
walidai kudhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi
na wanawake kushikwa sehemu za siri bila ridhaa yao."
Lembeli alitoa mfano kuwa Ali Nyenge
(38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa
maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanawe wa kiume
(11) akishuhudia huku akilazimishwa kuchora picha ya Chatu kwa kutumia
wembe kwenye paja lake.
Alisema mwanamke mmoja wa Babati (jina
tunalo) alidai kuvuliwa nguo na kulazimishwa kufanya mapenzi na wakwe
zake, pia kuingizwa chupa sehemu zake za siri.
Aidha, baadhi ya wanawake walidai
kubakwa na kulawitiwa huku wilayani Ulanga, mwanamke mmoja alidai
kubakwa na Askari wawili wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku.
No comments:
Post a Comment