Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza
Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi iliyofanya kuufikisha
mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya hapa ulipofika. Akizungumza
katika mahojiano maalumu na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya
Tume kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba Nape alisema;
“CCM inaipongeza Tume kwa kazi
waliofanya, tunatambua kazi kubwa waliyofanya, wamekamilisha kazi
waliyotumwa salama na kwa wakati. Sasa tuwaachie wanaondelea na mchakato
yaani bunge la katiba na hatimaye wananchi. Tunautakia kila lakheri
mchakato huu, utumike kutuunganisha watanzania badala ya kutugawa”
amesema Nape
Kuhusu pendekezo la Tume la muundo wa Muungano wa serikali tatu Nape anasema;
“Tumesikiliza hoja za tume juu ya
sababu za kuendelea kupendekeza muundo wa serikali tatu, tumezisikia,
tutazichukua,kuzipeleka kwenye vikao vya Chama baada ya tafakuri ya
kutosha tutaamua ipasavyo” alisisitiza Nape.
Aidha Nape alitumia nafasi hiyo kuwatakia watanzania kila lakheri kwenye mwaka mpya wa 2014.
No comments:
Post a Comment