Wafanyabiashara Jijini Mwanza wamefunga maduka yao na kuandamana wakizipinga mashine za risiti za kielektroniki za TRA.
Hata wale wakala wa magodoro na huduma nyingine zote wamejumuika kwenye mgomo huo. |
Hakuna huduma kabisa mitaa hii ambayo hukusanyisha wanunuzi wa mahitaji ya bidhaa mbalimbali.. |
Na maduka ya huduma kwa bidhaa za kielektoniki pamoja na vifaa vya kuendesha mashine na injini imesitishwa kupitia mgomo. |
Wafanya biashara wa vyombo vya elektoniki nao waunga mkono mgomo huo. |
Umekuwa kama mji wa kale uliokimbiwa. |
Hali hii imeathiri hata wauza magazeti kwani hakuna pilikapilika za wachuuzi na wanunuzi ambazo husababisha wao kupata wateja kwani ni bidhaa inayohitaji wapita njia.... |
Kweupeeeeee. |
Wafanyabiashara
wamekutana hapa katika kituo cha zamani cha mabasi cha Tanganyika
wakiwa na mabango yao yanayowasilisha ujumbe wa kukinzana na ujio wa
mashine hizo ambapo mbali na makato yake pia kodi nyingine hutozwa
pembeni hali wanayoitafsiri kama unyonyaji.
Jijini
Mwanza hususani eneo la katikati ya jiji barabara ya
Nyerere, Kenyata,
Lumumba, Libert na maeneo yote ya
wilaya ya Nyamagana leo wafanyabishara
wake katika
maeneo hayo waliingia katika mgomo wa kutofungua
maduka yao
kupingamashine za kutolea risiti za elektroniki
(EfDs) ambazo zipo katika mfumo wa uhakiki wa ukusanyaji
kodi.
Wafanyabishara
hao wamelalamika kuwa mbali na kuwepo
kwa mashine hizo za EfDs zinazo
hakiki mauzo yao na
utozaji kodi lakini pia wamekuwa wakiongezewa kodi
kila
kukicha.
Wamesema
kuwa matatizo ya mashine hizo ya kuharibika
mara kwa mara, kushindwa
kutoa mahesabu ya siku kwa
wakati na kushindwa kuprint risiti ni kero
kwao.
No comments:
Post a Comment