Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema imewavua
Uongozi Viongozi wake watatu baada ya Kugundua waraka wa Siri
uliowahusisha na mpango wa kukipasua Chama vipande vipande.
Viongozi waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini.
Viongozi waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini.
Akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari Mh Tundu Lissu
amesema katika Waraka huo kulikuwa na mtu anayejukana kama MM ambaye ni
Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni
Mwigamba na M2 hajajulikana ambaye ni mtumishi wa makao makuu ya
Chadema.
Mh Lissu amesema Dr Kitila Mkumbo alikana kabisa kumfahamu M2. Mh
Tundu Lissu anasema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi
unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini,
majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA.
Mh.Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu
Mh.Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu
No comments:
Post a Comment