Friday, November 22, 2013

HILI NDILO NEO LA WILLIAM NGELEJA KWA MH: ZITTO KABWE

Mhe Zito zuberi Kabwe natambua mchango wako mkubwa ulionao kwa taifa kama kiongozi kijana jasiri na shupavu tena usiyesita kusema kile unachokiamani kwa maslahi ya Taifa. Kuvunjika kwa pakacha sio mwisho wa uhunzi... Ziko fursa kubwa zaidi ambazo naimani unaweza ukazitumia kwa maslahi ya taifa nasio kwa masilahi ya wachache au chama kimoja cha chadema... 
Naimani ukifungua macho yako utabaini Mungu akiruhusu changamoto didi yako anatambua unauwezo wa kuikabiri, tena usijutie uwamuzi wowote wa hira au kwa kupanga dhidi yako ili utoke Chadema huu ni mpango na makusudi ya Mungu ili akufikishe hatua moja zaidi ambayo hauwezi ukaifanikisha ukizidi kuwepo chadema. Kwani naimani Mungu ariruhusu uwe kiongozi kijana ili ukamilishe kusudi la kuwatumikia watanzania hata kama ni kwa kupitia Chama kingine. 
Ila ukiweza kuja CCM chama chenye ukomavu wa kidemokrasia na sio domokrasia utakuwa umefanya maamuzi ya busara sanaaaa. Mungu wabariki viongozi vijana na Mungu ibariki Tanzania

No comments:

Zilizosomwa zaidi