Sunday, November 24, 2013

DK. KITILA MKUMBO AFUNGUKA, KUZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI MUDA WOWOTE

kitila_2f9e2.jpg
Tunawashukuru watanzania kwa kufuatilia kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Nawapa pole wote waliokwazwa na jambo hili, na ninawashukuru wote walionipa pole na kunitia moyo. Ninawashukuru pia walionilaumu na ni vizuri kunyosheana vidole na kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana kukwamisha harakati za mabadiliko.
Haya ni mawimbi katika harakati za mabadiliko na ninaamini yatapita na hayatayumbisha mchakato wa kusimika mfumo wa demokrasia hapa nchini kwetu.
Ninashauri tuwe na subira katika kutoa hitimisho na hukumu katika jambo hili. Mpaka sasa tumekwisha kupata upande mmoja juu ya kilichotokea. Vuteni subira nasi tuseme ndipo mpitishe hukumu.
 Mungu akijalia tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na tutaeleza upande wetu, na hasa kutoa maoni yetu juu ya kile kilichotamkwa jana kwamba sisi ni wahaini na wahujumu ndani ya chama chetu.
Kwa sasa tambueni tu kuwa mie binafsi bado nipo imara katika kuhakikisha kwamba siwi kikwazo na ninachangia kikamilifu nguvu zangu katika harakati takatifu za mabadiliko hapa nchini.

No comments:

Zilizosomwa zaidi