Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC
lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeumia
vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya
MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la
SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.Watu zaidi ya 35 wamepoteza maisha papo
hapo na wengika kujeruhiwa vibaya sana.kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo
eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4
ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano
lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna
daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa
basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni
gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka
kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini
kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine
linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi
kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndoho kulikuwa na watu
watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.Picha na Ahmad
Michuzi,Musoma.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda
Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni
ya J4 EXPRESS. Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 25 kupoteza maisha pamoja hapo.wakishuhudia tukio hilo la ajali.
Guldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano
lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka
kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki
dunia na mmoja kujeruhiwa.
Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.
Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.
No comments:
Post a Comment