Sunday, September 7, 2014

POLISI WAKAMATA BUNDUKI 8 BAADA YA MAJAMBAZI KUTEKA KITUO CHA POLISI

Baada ya tukio lililotokea juzi la majambazi kuvamia kituo cha polisi wilayani Bukombe na kuua askari wawili, tayari jeshi la polisi limeanza msako na kufanikiwa kukamata bunduki aina ya SMG 8, Pump action 1 na mtuhumiwa mmoja mwenyeji wa Tanga. Bado polisi wanaendelea na upelelezi na kuahidi kuwa Wote waliohusika katika tukio hilo Watapatikana muda si mrefu kuanzia sasa. Toeni taarifa kituo cha polisi kilicho karibu mara tu mnapomtilia mashaka mtu yeyote unayemhisi au kuwa na wasiwasi naye.

No comments: