Tuesday, September 16, 2014

KIJANA WA MIAKA 17 AFARIKI KATIKA SERENGETI FIESTA MKOANI SHINYANGA


Mwili wa marehemu Musa Shija mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa mtaa wa Mwalugoye kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga aliyeuawa kwa kushambuliwa akiwa kwenye Fiesta usiku wa ijumaa katika uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema uchunguzi wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.

No comments:

Zilizosomwa zaidi