Friday, July 11, 2014

DAKTARI FEKI AKAMATWA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO.

Huyo jamaa anatambuliwa kwa jina la Karume kauzu Habibu, anasadikika kuwa daktari feki aliyekamatwa  katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akitibu wagonjwa, amekuwa akivaa koti leupe mithiri ya  Daktari. kwa sasa anashikiliwa na polisi.

Amekutwa na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kinaonyesha anarudia mtihani katika kituo kimoja mjini Morogoro, ni mkazi wa Kigoma, kwa sasa alikuwa akiishi Liti manispaa ya Morogoro.

Polisi wanafanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Zilizosomwa zaidi