Azam FC yatwaa kwa mara ya pili Kombe la Mapinduzi  
Azam FC imeweza kutetea kombe hilo na kulibakisha 
nchini katika mchezo ulitumia dakika 120 kumalizika kwenye Uwanja wa 
Amaan, visiwani Zanzibar.
Goli la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC ndilo limeipatia ubingwa
 wa 
Kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo katika mchezo  ulimalizika
 kwa Azam FC kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Tusker 
FC ya Kenya.
 
 
Mabingwa hao kwa mara ya pili walipewa medali za dhahabu, kombe na 
kitita cha shilingi milioni kumi kama zawadi ya kutwaa ubingwa huo.
 
 Katika mchezo huo kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote bila 
kufungana, kipindi cha pili Tusker walianza kupata bao kupitia kwa 
mchezaji Jese Were aliyetumia uzembe wa beki ya Azam FC katika dakika ya
 59.
 
 Azam FC kupitia kwa beki wake mpya Jockins Atudo 
alisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Tusker 
Luke Ochieng kunawa mpira wakati akizui mpira wa kichwa uliopigwa na 
Mwaikimba, penati ilimriwa na mwamuzi Ramadhan Kibo.
 
 Goli hilo la kusawazisha kwa Atudo, ni goli lake la nne katika mashindano hayo, akifuatiwa na Mwaikimba mwenye magoli mawili.
 
 Matokeo ya sare ya 1-1 yalimaliza dakika 90, katika dakika za nyongeza 
Mwaikimba alitumia vema nafasi aliyoipata katika dakika ya 92 na 
kupachika goli hilo wavuni na kumaliza mchezo Azam FC ikitwaa ubingwa 
kwa ushindi wa 2-1.
 
 Baada ya goli hilo Azam FC walituliza mpira chini na kucheza mtindo wa kulinda lango lao kwa muda wote wa dakika 28 zilizobaki.
 
 Katika mchezo wa leo Azam FC walifanya mabadiliko mawili, walitoka 
Uhuru Seleman dk 64 nafasi yake ikachukuliwa na Abdalah Seif na dk 126 
aliingia Malika Ndeule kuchukua nafasi ya Brian Umony.
 
 Tusker 
walifanya mabadiliko walitoka Fredrick Onyango, Andrew Tololwa, Jese 
Were, Khalid Aucho na Ismail Dunga nafasi zao zikachukuliwa na Mark 
Odhiambo, Edwin Ombasa, Andrew Sekayambya, Benson Amianda na Michael 
Olunga.
 
 Baada ya kutwaa Kombe hilo, kocha mkuu wa Azam FC 
amewapongeza wachezaji wake kwa kubakisha kombe hilo na kusema ni 
muendelezo wa mipango ya mafanikio katika klabu hiyo.
 
 Amesema 
safari inaendelea ya kupeleka makombe katika klabu hiyo, walianza na 
Mapinduzi 2012, Ngao ya Hisani walilochukua nchini Congo DRC na hili la 
Mapinduzi 2013.
 
 Kikosi cha Azam FC kilichotwaa ubingwa, Mwadini
 Ally, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Jockins Atudo, 
Michael Bolou, Humprey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Uhuru 
Seleman/Seif Abdalah 64’ na Brian Umony/Malika Ndeule 126’.
 
 
Wengine waliokuwa na kikosi hicho, Aishi Salum, Wandwi Wiliam, Luckson 
Kakolaki, Omary Mtaki, Abdi Kassim ‘Babi’, Jabir Aziz, Ibrahim 
Mwaipopo,Salum Abubakar, Tchetche Kipre kabla ya kuumia,  waliokosa 
mashidano hayo ni Abdulhalim Humud, John Bocco, Waziri Salum ambao ni 
majeruhi.
Azam FC yatwaa kwa mara ya pili Kombe la Mapinduzi  Azam FC imeweza kutetea kombe hilo na kulibakisha nchini katika mchezo ulitumia dakika 120 kumalizika kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.
Goli la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC ndilo limeipatia ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo katika mchezo ulimalizika kwa Azam FC kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Tusker FC ya Kenya.
Mabingwa hao kwa mara ya pili walipewa medali za dhahabu, kombe na kitita cha shilingi milioni kumi kama zawadi ya kutwaa ubingwa huo.
Katika mchezo huo kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote bila kufungana, kipindi cha pili Tusker walianza kupata bao kupitia kwa mchezaji Jese Were aliyetumia uzembe wa beki ya Azam FC katika dakika ya 59.
Azam FC kupitia kwa beki wake mpya Jockins Atudo alisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Tusker Luke Ochieng kunawa mpira wakati akizui mpira wa kichwa uliopigwa na Mwaikimba, penati ilimriwa na mwamuzi Ramadhan Kibo.
Goli hilo la kusawazisha kwa Atudo, ni goli lake la nne katika mashindano hayo, akifuatiwa na Mwaikimba mwenye magoli mawili.
Matokeo ya sare ya 1-1 yalimaliza dakika 90, katika dakika za nyongeza Mwaikimba alitumia vema nafasi aliyoipata katika dakika ya 92 na kupachika goli hilo wavuni na kumaliza mchezo Azam FC ikitwaa ubingwa kwa ushindi wa 2-1.
Baada ya goli hilo Azam FC walituliza mpira chini na kucheza mtindo wa kulinda lango lao kwa muda wote wa dakika 28 zilizobaki.
Katika mchezo wa leo Azam FC walifanya mabadiliko mawili, walitoka Uhuru Seleman dk 64 nafasi yake ikachukuliwa na Abdalah Seif na dk 126 aliingia Malika Ndeule kuchukua nafasi ya Brian Umony.
Tusker walifanya mabadiliko walitoka Fredrick Onyango, Andrew Tololwa, Jese Were, Khalid Aucho na Ismail Dunga nafasi zao zikachukuliwa na Mark Odhiambo, Edwin Ombasa, Andrew Sekayambya, Benson Amianda na Michael Olunga.
Baada ya kutwaa Kombe hilo, kocha mkuu wa Azam FC amewapongeza wachezaji wake kwa kubakisha kombe hilo na kusema ni muendelezo wa mipango ya mafanikio katika klabu hiyo.
Amesema safari inaendelea ya kupeleka makombe katika klabu hiyo, walianza na Mapinduzi 2012, Ngao ya Hisani walilochukua nchini Congo DRC na hili la Mapinduzi 2013.
Kikosi cha Azam FC kilichotwaa ubingwa, Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Jockins Atudo, Michael Bolou, Humprey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Uhuru Seleman/Seif Abdalah 64’ na Brian Umony/Malika Ndeule 126’.
Wengine waliokuwa na kikosi hicho, Aishi Salum, Wandwi Wiliam, Luckson Kakolaki, Omary Mtaki, Abdi Kassim ‘Babi’, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo,Salum Abubakar, Tchetche Kipre kabla ya kuumia, waliokosa mashidano hayo ni Abdulhalim Humud, John Bocco, Waziri Salum ambao ni majeruhi.
No comments:
Post a Comment