
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Wazee wa kijiji cha
Majimoto kata ya Majimoto baada ya kupewa heshima ya kuwa Mzee wa Kijiji
hicho kwenye viwanja vya michezo vya Majimoto sehemu ambayo mkutano wa
hadhara ulifanyika na kuhudhuriwa na umati mkubwa.

Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasomea wakazi wa kijiji cha Majimoto
vijiji vitakavyopata umeme mwaka huu katika wilaya ya Mlele .

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Majimoto ambapo aliwaambia wapinzani wamekosa sera kabisa za kuzungumza
na kuanza kuwatukana waasisi wa Taifa hili akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere na kuwataka wananchi kutowapa nafasi wanasiasa
ambao hawana sera za maendeleo.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mama wa Waziri Mkuu
Pinda,Albertina Kasanga wengine waliongozana na Katibu Mkuu
alipomtembelea Mama wa Waziri Mkuu ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye ,Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Balozi Ali Abeid
Karume, Katibu Mkuu alifika kumsabahi Mama wa Waziri Mkuu wakati wa
ziara yake katika wilaya ya Mlele,aliyekaa kushoto kwa Mama ni mdogo wa
Waziri Mkuu Ndugu Wofgaga Pinda.
No comments:
Post a Comment