NA GODFREY MBAI
Hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Barani Ulaya
ilifikia tamati juma lililopita kwa timu nne kufanikiwa kufuzu hatua inayofuata
ya nusu ya michuano hiyo ambayo fainali yake itapigwa katika jiji la
Lisbon,Ureno.
Timu nne
zilizopata nafasi ya kucheza hatua ya nusu fainali msimu huu ni Atletico de
Madrid(Spain),Real Madrid(Spain),Bayern Munich(German) na Chelsea(England).Kati
ya timu hizo nne timu ya Atletico Madrid haikupewa nafasi kubwa ya kuweza
kufika katika hatua muhimu kama ya nusu
fainali msimu huu kwa kuwa imekua na rekodi mbaya katika michuano hiyo.
Lakini kwa weredi wa kocha wa timu hiyo,Muargentina
Diego Simeone na uwezo wa wachezaji wa timu hiyo,Atlectico Madrid sasa ipo mguu
mmoja kuelekea nchini Ureno kucheza fainali ya ligi ya mabingwa baada ya
kuwatupa nje ya mashindano wahispania wenzao,Barcelona katika hatua ya robo
fainali katikati ya wiki iliyopita kwa ushindi wa jumla ya magoli 2-1 baada ya
kucheza mechi mbili.
Ni wapenda soka wachache ulimwenguni walioipa nafasi
ya kufika mbali,huku wengi wakiami kuwa ingeishia katika hatua za makundi au
mikononi mwa Barcelona baada ya ratiba kuonyesha kuwa watacheza nao katika
hatua ya robo fainali.Kwa mujibu wa ratiba ya hatua ya nusu fainali iliyotolewa
na UEFA ijumaa iliyopita,Atlectico Madrid watacheza na Chelsea katika hatua
hiyo.
Kinachofanya mpaka kujiuliza,kuwa Atlectico Madrid
iliyoanzishwa 1903 kuwa wanaweza kuchukua ubingwa wa Ulaya msimu huu ni kwa
kuwa rekodi zinaonyesha kuwa kuanzia bingwa wa msimu wa 2006/2007 mpaka 2012/2013
wote waliifunga Barcelona katika hatua tofauti tofauti katika msimu ambao
Barcelona hawakuwa mabingwa katika michuano
hiyo yenye thamani kubwa duniani baada ya kombe la FIFA la dunia
Barcelona ilifungwa na Ac Milan katika hatua ya nusu
fainali msimu wa 2006/2007 na kufanikiwa kutwaa taji baada ya kuwafunga
Liverpool 2-1 katika fainali,mjini Athens,Ugiriki na msimu wa 2007,2008 Manchester
United walichukua taji baada ya kuwafunga Chelsea mjini Moscow,Urusi kwa
mikwaju ya penati na katika hatua ya nusu fainali waliwafunga Barcelona 1-0 Old
Trafford kwa mkwaju wa mbali wa kiungo Paul Schooles,mechi ya kwanza
iliisha 0-0.
2009/2010 Inter Milan ilikua bingwa baada ya
kuwafungwa Buyern Munich 2-0 katika dimba la Santiago Bernebeu,Spainlakini nao
katika hatua ya nusu fainali waliwafunga Barcelona enzi hizo Inter wakiwa chini
ya kocha Jose Mourihno. 2011/2012 Chelsea ilichukua ndoo baada ya kuwafunga
Bayern Munich katika fainali iliyoamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ta kwenda
1-1 katika dimba la Allianz Arena,Ujereumani.
2012.2013 ubingwa ulikwenda Ujerumani ambapo timu ya
Bayern Munich ilibeba kombe baada ya kuwafunga Wajerumani wenzao,Borrussia
Dortmund 2-0 katika fainali iliyopigwa katika uwanja wa Wembley,England.
Hivyo swali linabaki,je msimu huu Atletico Madrid
wataweza kufanya kile kilichofanywa na wengine kwa kuchukua ubingwa wa ulaya kupitia mgongo wa
Barcelona baada ya kuwafunga na kuwatupa nje ya michuano hiyo katika hatua
tofautit tofauti?
Nafasi ya Atletico kuweza kufanya hivyo ipo na hii
inatokana na jinsi timu hii ilivyojipanga msimu huu na hii inaonekana kwa jinsi wanavyocheza kwa
nidhamu kubwa katika mechi zao mbalimbali na licha ya kuwa katika hatua ya nusu
fainali ya ligi ya mabingwa msimu huu,pia kikosi hicho chenye nyota kama Diego
Costa,Koke,Joao Miranda na wengine wengi ,kipo katika mbio za kuwania ubingwa
wa Spain dhidi ya Barcelona na Real Madrid.
Hivyo muhimu ni kusubiri na kuona nini kitatokea kwa
Atletico de Madrid msimu huu? Hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya
itachezwa April 22 na 23 kwa Atletico Madrid kucheza na Chelsea wakati Bayern
watawavaa Real Madrid, huku mechi za marudiano ni wiki inayofuata.
No comments:
Post a Comment