
KASHESHE ILIANZIA HAPA
Makamu
mwenyekiti anatoa matangazo ya wageni wa wajumbe wa bunge maalum la katiba
pamoja na wageni wengine waalikwa.
Anasema
amepokea hati ya makubaliano ya muungano na ni certified copy.
Anamkaribisha
mh. Wassira aweze kutoa neno kuhusu hati hiyo.
Mh.
Steven Wassira, anasema hati hiyo ipo na ni halisi na ipo katika hali nzuri
hata baada ya kusainiwa miaka hamsini iliyopita.
Anasema
kuwa Tundu Lissu na wenzake walikutana baada ya kujua hati ipo na wakakubaliana
waseme saini ya Sheikh Karume sio ya kweli.
Anasema
watanzania tujihadhari na mawakala wa shetani.
Anasema
waasisi wetu wametukanwa sana mpaka kuitwa madikteta na hali hii haivumiliki
kwa watanzania wote.
Anasema
heshima ya waasisi wetu hailindwi na vyama bali inalindwa na italindwa na
watanzania wote.
Makamu
mwenyekiti,
Bunge
litaendelea Saa kumi jioni.
Anasitisha
kikao cha bunge maalum la katiba.
========
Bunge Maalum la Katiba, kikao cha jioni =======
Mh.
Anaanza
kwa kuunga mkono maoni ya wengi ambayo inatambua uwepo wa serikali mbili.
Anasema
zanzibar kuna makundi mawili yanayotaka mkataba na serikali mbili.
Sababu
za kuunga s2 ni kuwa muungano huu ni kuna kero za muda mrefu na anasema kuwa
kuna kero zishatatulika.
Serikali
ya tatu ya nini wakati kero zinatatulika.
Anasema
kuwa s3 haijaja lakini tayari ina kero 6,yanini kuwa muungano wa s3 ambayo
tayari ina kero sita wakati kero za s2 zinatatulika.
Anasema
cuf imefika bara na kumezwa na ukawa,wametoka zanzibar na asilimia 65 ya serikali
ya mkataba lakini walivyofika bara wakamezwa na chadema.
Anasema
chadema imewapa cuf majina tofauti na cuf wamejisahau kuwa chadema ndiyo
inayoibomoa zanzibar.
Anasema
amiri jeshi mkuu wa tanzania ni mmoja na ni rais wa JMT hivyo tundu lissu
asipotoshe.
Anasema
miaka hamsini hii ya muungano hawapaswi kustuka maana mtu mzima hatishiwi nyau.
Mh.
Mch. Ernest Kadiva
Anaanza
kwa kumshukuru Mungu.
Anasema
wanatakiwa kuunda katika ya wananchi wote na yenye misingi madhubuti ya
kusimamia nchi kwa muda mrefu.
Anasema
taifa linaeza kuporomoka muda wowote kama haina msingi ulio imara na hivyo
msingi lazima ulindwe.
Anasema
kuwa ili taifa liweze kuvunjika lazima ikatwe mizizi imara ya msingi wa taifa
hivyo taifa litatetereka.
Anapendekeza
kuwa JMT ni nchi inayomtambua Mungu,Isiyo na dini na isiyoruhusu uchafuzi
(kashfa) za kidini.
Anasema
dini ni msingi imara wa ustawi wa nchi.
Anasema
kama wosia wao bado una mantiki katika muundo huu wa serikali mbili basi bora
uenziwe.
Wananchi
wanataka kuona uchumi ulioimarika na mfumo watakaoutaka basi uhakikishe
unazingatia na namna ya kuimarisha uchumi ambacho ndo wananchi wanachotaka
kuona.
Mh.
Prof Lipumba
Anasema
yeye ni muumini wa dini ya mwenyezi Mungu hivyo ni muumini wa mapendekezo
yaliyoletwa na tume ya Warioba.
Anamnukuu
Lukuvi alivyoenda kanisani na kuwaasa waumini waupinge muundo wa S3 lasi hivyo
nchi itataliwa na jeshi,anasema Lukuvi aliwasilisha maoni ya Waziri mkuu.
Anasema
km zanzibar wangetaka muundo wa s1 moja basi wangekuwa na muundo wa serikali
moja lakini wazanzibar hawati muundo huo,anasema wanataka muungano utakaokuwa
na maridhiano.
Anasema
wanahitaji katiba itakayokuwa sawa kwa wananchi wote maana ndo msingi ulioachwa
na mwl Nyerere.
Anasema
ni fedhea kwa waziri kwenda kusema kanisani kuwa cuf zanzibar wanataka muungano
utakaoifanya zanzibar kuwa nchi ya kiislam.
Anasema
watatumiaje bajeti kubwa kukarabati ukumbi wakato wanajua katika hawaitaki.
Anasema
wamechoka ubaguzi na kudharau maoni ya wananchi.
Anasema
watu wote wanaokubaliana na maoni ya wananchi wanaondoka bungeni na kuwaacha
wao wajadili katiba wanayoitaka.
Wabunge
wengi wameondoka ndani ya ukumbi wa bunge na makamu mwenyekiti anasema kuwa
wakati wanaanza kikao cha bunge kolamu ilikuwa imetimia hivyo kanuni
inawaruhusu kuendelea na kikao.
Mh. Nyangwine Nyambari, Chanzo: Jamii forum
No comments:
Post a Comment