Kamanda Suleiman Kova
JAN ELOFF AKITOLEWA NJE YA
JAN ELOFF AKIHOJIWA NDANI YA CHUMBA MAALUM KILICHOPO NDANI YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY
Yule
mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae
amekamtwa kikomandoo akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki.
Habari
za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa South
Africa aliyefahamika kwa jina la JAN ELOFF ambae anaishi maeneo ya
Msasani Jijini Dar.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizonaswa na mtandao huu hatari kwa habari za
uchunguzi zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi
ya Euro hizo feki 700 mwandishi (jina kapuni) na DTV Bw. Livingstone
Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi
Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA
NJIA YA UDANGANYIFU,pamoja na Kutoa Euro Feki.
Baada
ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza
msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na
wadada wawili ambao ni raia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa
kitanzania ambao baada ya tukio la kukamatwa mwenzao wanaendelea
kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana
nao.
Kufuatia
kukamtwa kwa mzungu huyo wananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa
kufanikisha kukamatwa mzungu huyo. Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni
limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi kupigwa na mzungu huyo basi
wafike haraka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu
huyo.
No comments:
Post a Comment