Matokeo karibu yote yamekwisha kamilika nasi tunamsubiri msimamizi wa
uchaguzi Jimbo la Kalenga Bi Pudensiana Kisaka kumtangaza mshindi
ambaye bila shaka atakuwa ni Godfery Mgimwa wa CCM ambaye katika vituo
216 vya uchaguzi vilivyopigwa leo ameshinda kwa kiwango kikubwa dhibi ya
mshindani wake mkubwa Bi Grace Tendega Mvanda wa Chadema na Richard
Minja wa Chausta!Mgimwa ameshawasha taa ya kutangazwa mshindi,amemuacha
mbali sana Tengega!.....
Matukio ya kukupasha mwanajamvi
1.Wapiga kura wamekuwa wachache sana,waliojitokeza ni chini ya asilimia 50,sijui kwa nini watu hawajitokezi kupiga kura!
2.Waliojitokeza kupiga kura ni akina mama wenye umri kuanzia miaka
45,ambao katika vituo nilivyopita nikiwa na nimeambatana na waangalizi
wa ndani idadi ya vijana wa miaka 30 kurudi chini ilikuwa chini ya
asilimia 30.yaonekana wazee ndiyo wenye mwamko na siasa hapa Kalenga.
3.Baadhi ya vituo vya kupigia kura kuwekwa kwenye nyumba za watu,hili
nikiwa na waangalizi wa ndani tumelishuhudia katika kijiji cha kidamala
ambacho kituo kilikuwa sebuleni kwa Mzee Kinyondo ambapo hapo kuna Bar
pia,kwenye kata ya Luhoto kituo kilikuwa kwenye Grocery ya
Upendo,Kitongoji cha isakaleli,kituo kilikuwa nyumbani kwa mtu,kata ya
Nzihi,kituo kipo jengo moja na ofisi za CCM,kituo cha Malulumo kituo
tumekikuta nyumbani kwa bwana shamba,haya ni baadhi ya changamoto.
4.Wasimamizi walishindwa kuondoa mabango na bendera za wagombe na vyama
vya CCM na CHADEMA na kuacha watu wakapige kura huku nembo za vyama
zikiwa jirani na vituo.
5.Chama cha Chausta Pamoja na kutofanya
mkutano hata mmoja,kimeweza kuweka mawakala vituo vyote lakini mawakala
hawa walikuwa hata hawamjui mgombea wao na hata hawajawahi kumuona.
Nitawaletea uchambuzi wa uchaguzi huu kabla sijaondoka kuelekea
Chalinze,kwa sasa nipo ofisi za mkurugenzi nasubiri matokeo ya
mwisho,ila kumbuka mwanajamvi,mgombea wa CCM anaelekea kushinda kwa
kiwango kikubwa sana
Dotto Bulendu
No comments:
Post a Comment