Watu wawili wamekutwa wameuawa kikatili mchana wa leo katika matukio mawili tofauti Mkoani Shinyanga
Tukio la kwanza linamhusisha kijana ambaye jina lake halikufahamika lakini anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 ambaye amepokea kipigo kikali kutoka kwa raia wenye hasira kali kwa kupigwa mawe na fimbo na baadae kuchomwa moto kwa tuhuma za kuiba kuku wanne.
Tukio la pili ni la Bi Lucia Msunga mkazi wa kata ya Kizumbi ambaye amekutwa ameuawa kwa kuchinjwa kama kuku baada ya watu asiojulikana kumvamia usiku wa jana wakati akijiandaa kwa chakula cha usiku
kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Bw. Everist Mangala amethibitisha kutokea kwa matukio yote mawili na uchunguzi dhidi ya mauaji ya Bi.Lucia unaendelea.
Na Fatina M.
No comments:
Post a Comment