Tuesday, October 8, 2013

MGOMO WA MABASI KATIKA STENDI YA UBUNGO UMESABABISHA HALI HII

Hawa ni baadhi ya abiria wakiwa hawajui hatma ya safari zao.
Mabasi yaendayo mikoani leo asubuhi yamegoma kufanya safari zake kama ilivyo ratiba zake za kawaida, kwa madai kwamba walikuwa kwenye mgomo. Mabasi yote yalikuwa yamepakia abiria lakini hayakuwa yametoka kufuatia wamiliki wa mabasi hayo kuwakataza madereva kuyatoa mabasi hayo kama ilivyo kawaida. 
Mabasi hayo yamegoma kufuatia mgomo wa malori uliosababishwa na ongezeko la tozo la asilimia 5 katika mizani. 
 

No comments:

Zilizosomwa zaidi