Wayne Rooney |
Wayne Rooney amechapisha picha ya jeraha alilopata
kichwani baada ya wakosoaji wake kuhoji kujitolea kwake kuchezea timu ya
taifa.
Rooney alijeruhiwa na mchezaji mwenzake wa
Manchester United Phil Jones,kwa kumkanyaga kichwani na hivyo
kumlazimisha kukaa nje ya mechi za England kufuzu kushiriki kombe la
dunia zitakazochezwa Uijumaa na Jumanne.
Alisema kuwa baadhi ya watu
wanaonekana kuhoji kujitolea kwake na kusema kuwa amejiondoa kwenye
miuchuano ya kufuzu kwa kombe la dunia.
"nina uhakika watu wataona kwa nini sitaweza kucheza.''
Rooney, mwenye umri wa miaka 27, aliongeza kuwa
hakuna sababu inayoweza kumzuia kuwasaidia wachezaji wenzake kuweza
kufuzu kwa kombe la dunia.
Kocha mkuu wa Man United David Moyes alisema
kuwa Rooney huenda asicheze kwa wiki tatu kutokana na jeraha alilopata
Jumamosi kabla ya timu hiyo kushindwa na Liverpool, mechi ambayo Rooney
hakuweza kucheza kutokana na jeraha.
Mchezaji mwenzake wa timu ya taifa Theo Walcott
ameelezea kutishwa na picha hiyo akisema inafanana na picha
zinazoonekana tu kwenye filamu.
Rooney ni mmoja wa wachezaji watatu ambao wamejiondoa kutoka kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa sababu ya jeraha alilopata.
Wengine ni Glen Johnson na Jones.
No comments:
Post a Comment