Wednesday, September 4, 2013

WAKILI ISRAEL MAGESA AFARIKI GHAFLA

Israel Magesa
Wakili Magesa aliyeko  (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi.
Wakili Magesa, ambaye  ni mmiliki wa kampuni ya Mawakili ya Magesa &Co. Advocates, ni baba  mzazi wa Phares Magesa(MNEC),
Kalimba Magesa, Makongo Magesa, Yusuh (Yohana) Magesa, Rose Magesa, Salome Magesa, Emmanuel (Sospeter )Magesa , Marehemu Elisha Magesa (RIP) na baba Mkwe wa Haika Lawere.
Wakili Magesa enzi za uhai wake aliwahi kuwa Hakimu Mkazi Mkuu Mahakama ya Kisutu, Msajili wa Mahakama kanda ya kusini, Mwenyekiti wa Baraza la Nyumba Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Amnesty International - Tanzania Chapter, pia ni mmoja wa wanasiasa waanzilishi wa siasa za vyama vingi nchini.
Enzi za uhai wake alifanya kazi ya uhakimu Mkazi mikoa ya Singida, Kagera, Mtwara na Dar Es Salaam, na alikuwa ni miongoni mwa wanasheria waliomaliza shahada ya Sheria LLB katika Chuo Kikuu Cha East Africa miaka ya sabini mwanzoni na baadae kupata shahada ya Uzamili LLM toka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu Ukonga, Majumba Sita na shughuli rasmi ya kuaga itafanyika ijumaa tarehe 6/9/2013 kuanzia Saa 5 asubuhi Dares Salaam na mazishi yatafanyika siku ya jumapili 8/9/2013 kijijini Chitare, Majita, Musoma Vijijini.

No comments:

Zilizosomwa zaidi