MAFUTA YAKIWA NDANI YA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KABLA HALIJAONDOKA
MAFUTA YAKIWA NJE
GARI LIKIWA TAYARI KUONDOKA BAADA YA KUPAKIA MAFUTA
KIJAMPA KIKIWA KIMETULIA
ENEO HILI LILIKUWA LIMEFICHWA NA PLASTA ILI LISIJULIKANE KUWA NI LA WAGONJWA
HAPA LIKIWA LIMEFUNIKWA REBO KABLA YA KUGUNDULIKA
HAWA NDIO WALIOTOA MSAADA WA GARI HILO LA WAGONJWA LILILO GEUZWA KWA WIZI WA MAFUTA
HIZI NI PICHA ZA KUTHIBITISHA WIZI HUO WA MAFUTA
WATUHUMIWA tisa wa kesi ya wizi
wa mafuta katika mgodi wa Dhahabu( GEITA GOLD MINE ) kwakutumia gari la
wagonjwa (Ambulance) wafikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka matatu yanayowakabili.
Mwendesha mashitaka wa polisi
Inspekta Abiner ameiambia mahakama leo (9.9.213) kuwa mnamo 05/09/2013 saa 7:30 usiku uko
eneo la Geita power ndani ya mgodi wa geita gold mine watuhumiwa waliiba mafuta
lita 630 ya dizeli, kula njama za kuiba mafuta hayo kuaribu mali ambayo ni gari la kubeba
wagojwa katika kituo cha Afya cha Nzera kwakuling’oa viti
Mwendesha mashitaka amedai kuwa mtuhumiwa wa
kwanza Hamudi Biemo (28) Dereva wa gari hiyo anatuhumiwa na
makosa matatu likiwemo la kula njama na kung’oa viti vya gari hilo kwa lengo la
kubeba mafuta hayo mwendesha mashitaka huyo ameendelea kuiambia mahakama kuwa
watuhumiwa 8 wanakabiliwa na makosa 2 wizi wa mafuta na kula njama ya kuiba
mafuta hayo
Abiner ameongeza kuwa washitakiwa
hao walitumia gari aina ya Land Crusser yenye namba za usajili T 671 AKW mali ya
Halmashauri ya wilaya ya Geita nakuingia
mgodini nakuiba mafuta aina ya Diesel lita 630 zenye thamani ya Tsh. 1,386,000/=
mali ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)
Waliofikishwa
mahakamani ni Hamudi Biembo dereva
wa gari la wagonjwa ,Malemo Paul (31) mkazi wa mtaa wa Mseto
Geita,Selemani Magoso (31 )ambaye ni dereva pikipiki mkazi wa mtaa wa
Shilabela Geita,
Julias Boazi (28) mkazi wa Msalala road Geita )
Wengine ni Rashid Hussen (27) Mlizi wa mgodi, Ismail Zuber (26)mlinzi wa Kampuni ya G4S ,Christoper Kombo Operator wa GGM,Joseph Chiristopher (27) Operator wa GGM
Wengine ni Rashid Hussen (27) Mlizi wa mgodi, Ismail Zuber (26)mlinzi wa Kampuni ya G4S ,Christoper Kombo Operator wa GGM,Joseph Chiristopher (27) Operator wa GGM
Naye wakili wa upande wa utetezi
Bw. Leonard Bitemo baada ya watuhumiwa kusomewa mashitaka yao nakukana
mashitaka hayo wakili huyo aliiomba mahakama ya wilaya kuahirisha kesi hadi
wiki tatu ili wateja wake ambao ni Selemani Magoso, Boaz Paul na ,Milemo Paul wapate nafasi ya kujiandaa kwa ajili ya
utetezi.
Madai hayo yalipingwa na mwendesha mashtaka wa poisi
na kuomba mahakama ipange siku za karibu badala ya wiki tatu kwani kuna mashahidi ambao wanasafiri
kwenda nje ya nchi, kesi hiyo itajwe 12/09/2013 ambako
watakuwa wamejiandaa na mahakama ilikubaliana na uamuzi huo na wasitakiwa wote
(9) wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
Picha na Danice Stephano
No comments:
Post a Comment