Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuzingatia Kifungu
cha 3(2) Act NO. 8/1990 cha Sheria ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990
amewapandisha vyeo Maafisa wa Jeshi la Magereza 22 waliokuwa katika
ngazi ya Kamishna Msaidizi wa Magereza kuwa Makamishna Wasaidizi
Waandamizi wa Magereza.
Kwa
mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo Septemba 30, 2013 na Ofisi ya
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Makao Makuu ya Magereza, Dar es
Salaam inasema kuwa kupandishwa kwao vyeo hivyo kunaanzia tarehe 13
Septemba, 2013.
Aidha,
taarifa hiyo imeongeza kuwa taratibu za uvalishaji wa vyeo hivyo
zitafanyika katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga tarehe 5 Oktoba,
2013 saa 10:00 jioni.
Kufuatia
kupandishwa vyeo kwa Maafisa hao Kamishna Jenerali wa Magereza
Nchini(CGP) John Casmir Minja amewapongeza wale wote waliopandishwa vyeo
na kuwataka kuendelea kutenda kazi zao kwa ubunifu, kasi zaidi na
ufanisi ili waendelee kuongezewa Madaraka zaidi. Aidha Madaraka hayo
waliyopewa ni miongoni mwa mikakati inayoendelea hivi sasa katika
Maboresho ya kulijenga Jeshi la Magereza kuwa la Kisasa ili liweze
kutekeleza majukumu yake kwa Weledi zaidi.
Imetolewa na Inspekta Lucas Mboje,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
Tarehe 30 Septemba, 2013.
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
Tarehe 30 Septemba, 2013.
No comments:
Post a Comment