Sunday, September 15, 2013

HAYA NDIO MAAMUZI MAPYA YA UHURU, KAGAME NA MUSEVENI



Wiki iliyopita Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Rwanda, Paul Kagame walikutana Mombasa nchini Kenya na kuzindua mradi mkubwa wa ujenzi wa reli.


Katika uzinduzi huo marais hao wameweka muda wa kuanza kwa miradi mitatu mikubwa, mosi kuanza kwa mradi wa ujenzi wa reli kutoka Mombasa-Kampala mpaka Kigali, ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Eldoret-Kampala mpaka Kigali na kujenga miundombinu ya umeme wa uhakika.

Pia marais hao wamewaagiza mawaziri wa fedha wa nchi hizo kuandaa mapendekezo ya utekelezaji wa miradi hiyo mitatu na taarifa ya mapendekezo hayo wataitoa kwa marais hao katika mkutano ujao.


Kwa mujibu wa mratibu wa miradi hiyo, Monique Mukaruliza, ujenzi wa bomba la kusafisha mafuta kutoka Eldoret-Kampala mpaka Kigali, unatarajiwa kukamilika 2017 huku kabla ya mwisho mwa mwaka huu, viongozi wa  nchi hizo wakubaliana kuzindua ushuru wa pamoja wa forodha kwa ajili ya kusafirisha bidhaa kwa masharti nafuu kutoka nchbi moja hadi nyingine.

Ujenzi wa Reli Kuanza Novemba

Wakati hayo yakiendelea, taarifa zinaeleza kuwa ujenzi wa reli hiyo utagharimu dola 3.5 bilioni na mradi huo utakamilika mwaka 2018 huku ujenzi wa awali wa mradi wa reli kutoka Mombasa mpaka jijini Nairobi unatarajiwa kuanza Novemba, mwaka huu.

Vilevile kuanzia Januari mwakani,  Rais wa Kenya, Kenyatta na Kagame wamekubaliana kwamba wananchi wao waanze kutumia vitambulisho vya uraia kusafiria katika nchi hizo wakati Uganda itatumia kadi ya kupiga kura kusafiri Kenya na Rwanda. 


Mbali na hayo taarifa iliyotolewa hivi imebainisha kwamba katika mkutano wa pili uliofanyika Mombasa wiki iliyopita, marais hao waliwaagiza mawaziri wa fedha wa nchi hizo kuandaa mapandekezo ya utekelezaji wa miradi hiyo ndani ya mwezi mmoja na nusu.


Wataalamu wa masuala ya uchumi, anabainisha kwamba reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba mizigo na kukimbia kilometa 80 kwa saa wakati ikapoanza kusafirisha mizikgo katika ukanda huo.


Bandari ya Mombasa, inategemewa kwa zaidi ya asilimia 50 na Rwanda katika kuagiza mizigo huku wakati huo huo ikitegemewa na Uganda, Mashariki mwa Demokrasia ya Konga (DRC), Burundi, Kaskazini mwa mikoa ya Tanzania na Sudani Kusini.


Burundi na Sudani Kusini

Katika mkutano huo marasi wa nchi hizo tatu walikubali kuijumuisha Burundi na The Presidents agreed to consider Burundi na Sudani Kusini miradi hiyo baada ya kuudhuria mkutano huo kama wageni waalikwa.


Kutokana na makubaliano hayo ni dhahiri kwamba nchi hizo tano zimekubaliana kufanya kazi pamoja katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa nchi hizo kiuchumi.


“Wawakilishi wa Burundi na Sudani Kusini wanapaswa kuwa sehemu ya miradi hiyo na hasa katika kamati za ufundi," inaeleza sehemu taarifa ya mkutano huo.

Mukaruliza anabainisha kwamba Burundi na Sudani Kusini walialikwa kwenye mkutano huo kama watamazaji na baadaye waliomba kuwa sehemu ya juhudi za kuanzisha miradi hiyo.

Katika mkutano huo Rais Kenyatta alitoa taarifa ya maendeleo ya miradi hiyo iliyotokana na mkutano uliofanyika  Entebbe, Juni mwaka huo.

“Ninayo furaha kutoa taarifa ya mradi wa bomba la mafuta na katika hatua ya kwanza ya maendeleo ya mradi wa bomba la mafuta, unaendelea vizuri na hatua ya awali tayari imeanza na upembuzi yakinifu umekamilika," anasema Rais Kenyatta.

Pia Kenyatta anasema kwamba kuna changamoto zinazokabili nchi hizo na kwamba wanapaswa kuungana pamoja kwa ajili ya kuzishinda na kufikia malengo yaliokusudiwa.

Kuhusu hati za kuruhusu watu wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuingia katika nchi moja hadi nyingine, katika mkutano huo suala hilo lilijadiliwa na mkutano uliwaagiza mawaziri husika kutoa taarifa kwa nchi ya Kenya, Rwanda na Uganda katika mkutano wa tatu utakaofanyika Oktoba mwaka huu ili mpango huo uanze Januari mosi, mwakani.

Vilevile mawaziri husika wameagizwa kukamilisha mchakato wa kutumia vitambulisho vya uraia kabla ya Oktoba, mwaka huu ili vitumike kama hati rasmi kusafiria katika nchi hizo Januari mosi, mwaka huu.

Katika mkutano huo, Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir Mayardit aliwakilishwa na waziri wake wa masuala nje, by , Dk Barnaba Marial Benjamin wakati waziri wa usafirishajiwa Burundi, Deogratias Rurimunzu alimwakilisha  the rais Pierre Nkurunziza.

Mkutano mwingine utafanyika Oktoba mwaka huu jijini Kigali.

No comments:

Zilizosomwa zaidi