JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUREJESHWA KWA URUSHAJI MATANGAZO RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO
1.0 Utangulizi:
Mnamo
tarehe 26/02/2013 Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
ilitoa uamuzi wa kuvifungia vituo vya utangazaji vya Radio Imaan ya
mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kukiuka
Sheria na Kanuni za Utangazaji.
Kamati
ya Maudhui iliuita uongozi wa vituo hivyo tarehe 11/02/2013 na tarehe
14/02/2013 ili kujitetea na vyote vilikiri kosa. Baada ya kutafakari
utetezi wa Radio Imaan na Radio ya Kwa Neema FM na kwa kuzingatia Sheria
na Kanuni za Utangazaji, Kamati iliamua kutoa adhabu kwa vituo vyote
viliwi kama ifuatavyo:-
a) Vituo vyote vilipewa onyo pamoja na kufungiwa kurusha matangazo kwa kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe 26/02/2013;
b) Vituo
vyote vilitakiwa kuithibitishia Mamlaka ya Mawasiliano na Kamati ya
Maudhui kwa maandishi kuwa hawatarejea kutenda kosa la aina hiyo au
linalofanana na hilo. Ikiwa vitarudia Kamati ya Maudhui haitasita
kuvifutia leseni zao za utangazaji.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
2.0 Kutekeleza adhabu na hatua zilizochukuliwa na vituo hivyo
na Mamlaka ya Mawasiliano:
Baada
ya Uamuzi huo kusomwa, vituo vyote viwili vilianza kutekeleza adhabu
mara moja kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za
Utangazaji. Mamlaka ya Mawasiliano ilipokea barua ya udhibitisho wa
kutofanya kosa tena yaani “Commitment letter” pamoja na sera ya uhariri
(Editorial Policy) na ratiba ya vipindi kutoka kwa vituo vyote viwili.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania ilifanya ukaguzi kwa vituo vyote viwili ili
kujiridhisha na kuzipitia sera za uhariri pamoja na mwongozo wa vipindi
kabla ya kuvifungulia.
3.0 Kurejeshwa kwa Matangazo
Kamati
ya Maudhui iliandika barua tarehe 27/08/2013 kuhusu kuvifungulia vituo
hivyo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM
Radio ya jijini Mwanza baada ya kutumikia adhabu kwa mujibu wa Sheria na
Kanuni za Utangazaji. Vituo hivi vimeanza kurusha matangazo yake
kuanzia leo tarehe 28/08/2013 baada ya muda wa adhabu kuisha.
Kamati
ya Maudhui inapenda kutumia fursa hii kuvionya vyombo vya habari vya
utangazaji vya redio na televisheni kuwa makini katika kutekeleza
masharti ya leseni pamoja na kufuata Sheria na Kanuni za Utangazaji.
Kamati ya Maudhui haitasita kutoa adhabu kali au kuvifungia vituo
vitakavyokiuka Masharti ya leseni, Sheria pamoja na Kanuni za Utangazaji
au hata kuvifutia leseni zao.
Kamati
ya Maudhui inatoa wito kwa vyombo vya habari vya utangazaji kuzingatia
Sheria, Kanuni na Masharti ya leseni ilikuboresha Sekta ya Utangazaji na
kudumisha amani nchini.
Eng. Margaret Munyagi
Mwenyekiti,
Kamati ya Maudhui Ya TCRA,
S.L.P. 474,
DAR ES SALAAM.
28/08/2013
Mwenyekiti,
Kamati ya Maudhui Ya TCRA,
S.L.P. 474,
DAR ES SALAAM.
28/08/2013
No comments:
Post a Comment