Wakazi wa Mbezi Beach, Tegeta na Wazo
katika Manispaa ya Kinondoni wamelalamikia kazi ya ubomoaji wa nyumba
zao ili kupisha utandazaji wa bomba la majisafi la Mamlaka ya Majisafi
na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), kwamba inafanywa kwa ubaguzi.Hata
hivyo, ilielezwa kuwa Dawasa ilitoa siku 14 kwa wakazi hao kubomoa
nyumba zao zipatazo 400 kupisha mradi huo wa bomba utakaogharimu Sh120
bilioni.(P.T)
Dawasa imelaumiwa kutokana na baadhi
ya nyumba za vigogo na watumishi wa Serikali kuachwa licha ya kuwekewa
alama ya X kuashiria zinatakiwa kubomolewa.
Mwandishi wa Mwananchi aliyekuwa eneo
la tukio, alishuhudia baadhi ya wananchi hao wakidai kuwa moja ya nyumba
ambayo imeachwa ni ya ndugu wa mmoja wa vigogo wa Serikali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana
huku ubomoaji ukiendelea, mmoja wa waathirika wa bomoabomoa hiyo,
alilalamikia ubomoaji kufanyika kibaguzi.
Juma Shaaban alisema: "Ninashangaa
kuona tunabomolewa nyumba zetu huku nyumba zao zinaachwa,"Ninaweza
kukuonyesha nyumba ya ndugu yake kigogo (anamtaja) imewekewa X, lakini
chakushangaza haijabomolewa, hii tulalamike."alisema.
Mkazi mwingine wa Tegeta, Khamis
Ramadhani alisema: "Tunashangazwa na bomoabomoa hii kufanyika bila hata
kutupa muda wa kuhamisha mali zetu."
Katika hatua nyingine, bomoabomoa
inayoendelea ilisababisha hitilafu ya umeme na kusababisha moto
ulioteketeza Baa maarufuya Samaki Samaki.
Moto huo ulitokea Saa 4 asubuhi na
kusababisha watu kujaa na kufungwa barabara kwa muda ili kuzima moto huo
kabla ya magari ya kuzima moto kuwasili eneo la tukio
No comments:
Post a Comment