Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari
ndogo waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka huko katika barabara kuu
ya Bagamoyo Dar esalaam
Ajali
hiyo ilitokea jana Septemba mosi majira ya saa moja asubuhi na kwamba watu hao
wawili waliopoteza maisha mmoja ni mfanyakazi wa Benki ya CRDB na mwingine ni
mtumishi wa benki ya Akiba(Akiba bank) wote wakazi wa jijini Dar salaam.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo Idrisa Shaban na Shida Mzee wakazi wa kijiji
cha Matumbi Bagamoyo, wamesema ajali hiyo imehusisha gari T 845 ANB Toyota
Hilux na tukio hilo limetokea baada ya kupasuka gurudumu la mbele kushoto
kisha kulivuta gari mtaroni na kupinduka.
Kamanda
wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei amethibitisha ajali hiyo na kutaja gari
iliyohusika ni Toyota Hilux mali ya Paulo Mutaganjwa na kwamba ilikuwa
ikiendeshwa na George Beda mfanyakazi wa kampuni ya Coca Cola.
Matei
amesema katika tukio hilo watu wawili walikufa na tisa kujeruhiwa na
kwamba waliokufa ni William Temu (30) na Stella Godwin wote wafanyakazi wa
benki hizo na wakzi wa Dar salaam.
Matei
amewataja majeruhi waliotambulika majina ni Vivi Mbwambo(27) mfanyakazi wa DSTV
Mlimani City Dar esalaam, Neema Bernad(31) mfanyakazi wa kampuni ya simu za
mkoni ya TIGO Dar esalam, Godwin Bernad mfanyakazi wa Bandarini Dar esalam,
Wengine
waliojeruhiwa ni dereva Beda, Glory Somi (30) mfanyabiashara, Hegela Nkya(34)
mfanyabiashara, Joyce Muro(34) mfanyabiashara wote wakazi wa Dar salaam na wote
walikuwa wakisafiri na gari hilo.
Kamanda
Matei amesema majeruhi wote mara baada ya kuokolewa walipelekwa katika
hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya matibabu na kwamba miili ya
marehemu hao nayo ilipelekwa kuhifadhiwa hapo.
No comments:
Post a Comment