
Kitu kingine ni jinsi kocha mpya Gerardo 'Tata' Martino
atakavyoweza kuonesha uwezo wake na kuipa mafanikio Barcelona kama ilivyokua
kwa makocha waliopita.
Kocha huyu Muargentina aliteuliwa mapema mwezi uliopita
kuchukua nafasi ya Tito
Vilanova msaidizi wa zamani wa Pep Guardiola
kutokana na matatizo ya kiafya yaliyomfanya kuachia ngazi na kushindwa kuendelea kuinoa timu hiyo Ingawa uteuzi wake haukutegemewa na wengi.
Kocha huyu kabla ya kujiunga na Barcelona alikua akiinoa
timu ya zamani ya Lionel
Messi ya Newell's Old Boys.
Barcelona
imewapoteza nyota wake akiwemo straika David Villa aliyejiunga na Atletico Madrid,
pamoja na Thiago Alcantara aliyetimkia Bayern Munich. Mabingwa hao wa Hispania
wametumia €57 million kumnasa kinda wa Kibrazil Neymar mwenye umri wa miaka 21.
Neymar mefunga magoli mengi wakati wa mechi za majaribio na ameonekana akizoeana
vizuri na wachezaji wenzake. Kinda huyo ameahidi kufanya vizuri na kuonesha
ubora wake zaidi.
Na Mligo G
No comments:
Post a Comment