Ingawa matokeo hayo yameonekana kama aibu kwa
timu inayoshika nafasi ya kwanza kwa ubora barani Africa, tembo hao waliwakosa
baadhi ya wachezaji wao nyota akiwemo Yaya Toure ambaye ndiye mchezaji bora wa
mwaka barani Africa. Kocha Ivory Coast Mfaransa Sabri Lamouchi aliwaacha benchi baadhi ya wachezaji
wenye majina makubwa, hadi pale walipoingizwa madhara yalikuwa yamekwisha
igharimu timu.
Baada ya kuondoka
Chelsea na kwenda China kulimgharimu Drogba kutokana na kiwango kidogo cha soka
eneo hilo, hali iliyopelekea kuonesha kiwango cha chini wakati wa michuano ya
kombe la mataifa Africa mwanzoni mwa mwaka huu nchini Afrika Kusini. Mara baada
ya kushindwa kuchukua kombe hilo kitu cha kwanza alichokifanya kocha Lamouchi ilikua
ni kumwacha Drogba katika kikosi chake na kumwambia aboreshe kiwango chake.
Drogba ameonekana kurudi
katika kiwango chake hasa baada ya kutoka nchini China na kutimkia Uturuki kitu
kilichomfanya kocha Lamouchi kumjumuisha kwenye kikosi cha jana katika mechi ya
kirafiki. Bila shaka sasa Drogba anamatumaini ya kuiitwa tena kikosini kuelekea
mpambano wao dhidi ya Morocco mwezi Septemba kuwania kufuza kucheza fainali za
kombe la Dunia nchini Brazil hapo mwakani.
Na Mligo G.
Na Mligo G.
No comments:
Post a Comment