

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Vodacom, Yanga Sports Club na makamu bingwa Azam FC wanatarajia kuvaana kesho (Jumamosi) kwenye
mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa
2013/2014.
Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo mshindi atakabidhiwa ngao.
Iwapo dakika 90 za mechi hiyo
hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa mikwaju ya penalti huku
asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda kwa kituo cha kulelea watoto cha
SOS.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa
sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa
ni Sh10,000. Watakaiongia viti Maalum yaani VIP ( C) watalipa Sh15,000, viti vya VIP (B) ni
Sh20,000 wakati VIP (A) watalipa Sh30,000.
Na Mligo G
No comments:
Post a Comment