VURUGU
na mizengwe vimeendelea kuandama uchaguzi ndani ya CCM, baada ya Katibu
wa CCM mkoani Arusha, Mary Chatanda kunusurika kupigwa katika uchaguzi
wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Katibu huyo alinusurika kipigo baada ya kutuhumiwa kutaka kuuvuruga uchaguzi huo wa kumpata mwenyekiti wa vijana mkoa.
Baadhi
ya wajumbe wa mkutano huo walimtuhumu Chatanda kuwa alitaka kuuvuruga
ili ampitishe mgombea ambaye ni chaguo lake aliyetajwa kwa jina la Dk
Harold Adamson.
Katika vurugu hizo, Chatanda
alinusurika kupigwa na wajumbe waliotoka Wilaya ya Monduli ambao
walitaka uchaguzi urudiwe ili haki itendeke.
Dalili za
kuibuka kwa vurugu zilianza kujitokeza mapema baada ya makundi ya
baadhi ya vigogo wa CCM yanayohusishwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward
Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernad Membe kutambiana nje ya ukumbi
wa mkutano.
| |
Wednesday, October 10, 2012
Uchaguzi UVCCM Arusha ni vurugu tupu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Kwa wasiomfahamu, Davido ndio kama Diamond Platnums wa Nigeria kwa sasa, ni mshkaji mdogo ambae ametoka kwenye familia iliyoshika din...
-
1.AUSTIN MORRIS A-40 AUSTIN MORRIS A-40 Gari aina ya Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 ...
-
Jeraha katika mguu wa mwandishi wa habari Shomi Mtaki lililotokana na risasi baada ya kuvamiwa na majambazi Shomi Mtaki akione...
-
Valladolid 1 - 1 Valencia Athletic Bilbao 2 - 1 Sevilla FC Mallorca 2 - 4 Barcelona Atlético Madrid 2 - 0 Getafe Levante 1 - 2 Real Mad...
-
Mganga wa kienyeji mkazi wa Kijiji cha Nyansincha, wilayani Tarime mkoani Mara, Mwita Nyamankore, anasakwa na Polisi kwa madai ya kum...
No comments:
Post a Comment