Habari ifuatayo imeandikwa na Ramadhan Ali na Mwanaisha Mohammed
Askari mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105
Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa
kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi wakati akirudi kazini
majira ya saa 6.30 usiku katika eneo la Bububu.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Ziwani, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa
amesema mauaji hayo yamesababishwa na fujo za wafuasi wa Jumuiya ya
UAMSHO baada ya kuenea uvumi wa kutekwa Msemaji Mkuu wa Jumuiya hiyo
Sheikh Farid Hadi usiku wa kuamkia jana.
Kamishna Mussa amesema Jeshi la Polisi
linaendelea na msako wa kuwatafuta watu waliofanya mauaji ya Coplo Saidi
Abdulrahaman ili kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani kama sheria za
nchi zinavyowaelekeza.
Amesema mpaka hivi sasa watu 10
wamekamatwa kwa tuhuma za makosa mbali mbali yaliyotokana na vurugu za
jana na upelelezi wa kujua ukweli juu ya uvumi wa kutekwa Sheikh Farid
unaendelea.
Ameongeza kuwa kutekwa kwa Sheikh Farid
kunatia mashaka kutokana na mazingira ya kutoweka kwake kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na mdogo wake Said Omar Said ambae alikuwa dereva
wake katika hatua za mwisho maeneo ya Mazizini walipokwenda kununua
umeme.
“Sheikh Farid alimuamuru Said amuache
katika eneo hilo aende nyumbani kupeleka umeme na wakati huo akaendelea
na mazungumzo na watu wengine walikuwemo ndani ya gari nyengine ndogo ya
NOAH ambayo nambari zake hazijajulikana lakini aliporudi kumchukua
hakumkuta” alisema Kamishana Mussa.
Amesema fujo hizo zilisababisha hasara
kubwa kwa Serikali, Chama tawala na wananchi ikiwemo kuchoma na
kuharibumiundo mbinu ya barabara, kuharibu maskani za CCM za Kisonge na
Muembeladu kwa kuzichoma moto baadhi ya magari kuvunjwa vioo na kuvunja
duka la pombe na kuiba mali iliyokuwemo ndani.
Hata hivyo amedai hali ya Mji wa
Zanzibar kwa sasa ni shwari, wananchi wanaendelea na shughuli zao kama
kawaida na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikosi vyengine vya
ulinzi na usalama vitaendelea kuhakikisha amani inadumu muda wote.
Amewataka wananchi kuendelea kuwa
wavumilivu na kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao, na kutoa
taarifa za watu waliohusika na vurugu pamoja na mauaji ya Coplo Said
Abdulrahaman.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Meja Eric Komba akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam...
-
-
Mtangazaji wa ITV anayejulikana kwa jina la Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye pia alimuu na...
-
Matukio ya wananchi kumwagiwa tindikali yameendelea kushika kasi nchini baada ya Mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi, Christian Msema wa M...
-
Ernest Mangu TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ju...
No comments:
Post a Comment