Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim,Majaliwa akipokea
tuzo ya filamu kutoka kwa msanii Single Mtambalike aliyoshinda katika
Tuzo za Filamu Afrika kwa mwaka 2016 zilizofanyika chini Nigeria hivi
karibuni kulia ni msanii Elizabeth Michael.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim,Majaliwa (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Filamu Afrika kwa
mwaka 2016 pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe. Annastazia Wambura(wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Grabriel(wa pili kushoto),
kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso na kushoto
ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imefarijaka kwa ushindi wa
wasanii wa filamu nchini walioshinda tuzo za filamu Afrika za mwaka
2016(African Magic Viewers Choice Award) ziliyofanyika jijini Lagos
nchini Nigeria mwishoni wa wiki iliyopita.
Waziri
Mkuu Majaliwa, amesema hayo leo katika ukumbi wa mikutano ulipo katika
Ofisi yake Jijini Dares Salaam, alipokutana na washindi wa tuzo za
filamu Afrika za mwaka 2016 (AMVCA) ambao ni Elizabeth Michael ‘Lulu’
aliyeshinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki na Single
Mtambalike ‘Richie’ aliyeshinda tuzo ya Filamu Bora ya Kiswahili pamoja
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Annastazia
Wambura,Katibu Mkuu wa wizara Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso na wasanii wa filamu.
“Serikali
imefarijika sana kwa nyie kwenda Nigeria na kushinda na mmetumia lugha
ya Kiswahili, lazima tutumie nafasi hii kuwatangaza pia mmuendelee na
fani hii ili kuvutia wengi zaidi” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Aidha,
Waziri Mkuu amewapongeza wasanii hao na kusema kuwa Serikali itaendelea
kushirikiana na wasanii wakati wowote na amewataka kujipanga vizuri
kutumia vyama vyao vya sanaa na kusisitiza kuwa Mhe. Rais John Pombe
Magufuli ametoa matamko kadhaa kuhusu sanaa na wasanii na ameendelea
kushughulikia malalamiko yao ikiwemo suala la COSOTA, na kusema kuwa
baada ya taratibu zote kukamilika suala hilo litasimamiwa na Wizara
inayohusika na kazi za Sanaa.
Waziri
Mkuu Majaliwa, pia amewataka watanzania kuacha tabia ya kutojiamini na
kujidharau, na kuwataka watu waige mfano kwa wasanii hao, na kuwashauri
wasanii wote kwa ujumla kutumia vyombo vya habari kujiimarisha na
kujitangaza.
Kwa
upande wao, wasanii waliopata tuzo hizo kwa filamu ya “mapenzi ya
Mungu” ya Elizabeth Michael na filamu ya “Kitendawili” ya Single
Mtambalike, wameishukuru Serikali kwa kuwathamini na kuonesha
ushirikiano katika kazi zao za sanaa, na wameahidi
kuendelea kutengeneza kazi nzuri za sanaa ili ziweze kuitangaza
Tanzania kimataifa.
Naye,
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Saimon Mwakifamba
ameishukuru Serikali kwa jitihada mbalimbali inazofanya katika kusaidia
tasnia ya sanaa kwa ujumla na ameahidi kuendelea kushirikiana na
Serikali katika kuendeleza tasnia hiyo kimataifa.
No comments:
Post a Comment