Mgombea
Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga
Wananchi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kumaliza
kujitambulisha na kuwashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kuchaguliwa kwake
katika nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake kuwania nafasi ya
Urais .
Mbunge wa
Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe
Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi
kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani
Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji
hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli
ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa
zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
Baadhi ya
Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika
kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.
Baadhi ya
Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa
wingi kumlaki Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi
CCM,Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo
na shamra shamra za mapokezi kurindima kila kona wakifurahia uteuzi wa
CCM kwa Dkt Magufuli,huku wengine wakiwa wamebeba mabango kama hivyo
pichani.
Mbunge wa
Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe
Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi
kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani
Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji
hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli
ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa
zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
Naibu Katibu
Mkuu wa CCM (Bara),Ndugu Rajab Luhwavi akiwasalimia wanachama wa CCM
pamoja na Wananchi waliofika kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo katika
kituo cha mabasi cha zamani ndani ya wilaya hiyo.
Ilikuwa ni shangwe tu jioni ya leo ndani ya Wilaya ya Chato ambako ndiko nyumbani kwa Mbunge na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli.
Mbunge wa
Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe
Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji wa Katoro mkoani Geita alipokuwa
akipita njiani kuelekea wilayani Chato.Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli
mkoani humo wananchi walijitokeza kwa wingi kila baada ya kilometa
kadhaa na kuziba barabara wakita kumuona Dkt Magufuli na kumpongeza kwa
kuchaguliwa kwake na chama cha CCM.
Mwananchi
akiwa amekumbwa na joto la furaha mara baada ya kumuona Dkt Jonh
Magufuli akiwa na msafara mzima wakielekea jimboni kwake Chato mkoani
Geita.
Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza Mh.Magesse Mulongo akiwasalimia wananchi wa Chato jioni ya
leo,kabla ya kumkaribisha Dkt John Magufuli aliyewasili mjini humo jioni
ya leo akitokea mkoani Mwanza akijitambulisha kwa wananchi na
kuwashukuru.
Dkt Magufuli akizungumza jambo kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Chato jioni ya leo
Dkt Magufuli akifurahia jambo mbele ya umati wa watu,mara baada ya kujitambulisha kwao.
Mgombea
Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru
wakazi wa mji huo kwa kujitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya
kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita
kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao
walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa
Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila
pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
Maelfu ya Watu walijitokeza kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo mjini Chato mkoani Geita.
PICHA NA MICHUZI JR-CHATO-GEITA
No comments:
Post a Comment